TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION

TANGAZO SHIWATA

Friday 20 March 2015

SHIWATA yaomba wasanii wapige kura ya maoni Katiba Mpya

Na Peter Mwenda

MTANDAO wa Wasanii Tanzania (SHIWATA)umeipongeza Serikali kwa juhudi zake za kuandaa katiba mpya na kuunga mkono mapendekezo kwa unawaomba wanachama wakewaipigie kura ya ndiyo kwani ni mkombozi wa wasanii.

Mwenyekiti wa SHIWATA, Caasim Taaliba alisema jana kuwa Serikali imetutambua rasmi wasanii na kusikiliza kilio chao cha muda mrefu na hasa kuhusu wizi wa kazi zao ambavyo vimeingizwa kwenye katiba hiyo.

Alisema SHIWATA yenye wanachama 8,000 ikiwa imetimiza miaka kumi imewataka wasanii kutafakari namna ya kujikomboa kupitia katiba hiyo.

Katika hatua nyingine SHIWATA imesema imefanikiwa kujenga nyumba 104 katika kijiji cha wasanii cha Mwanzega, Mkuranga mkoa wa Pwani na kuanza kilimo kwanza katika kijiji cha Ngarambe.

 Alisema mtandao huo unasikitishwa na taarifa ambazo siyo za kweli kuwa ndani mtandao huo kuna utapeli na kuongeza kuwa wanataarifu wanachama wo wote kwamba mpango
huo ni wa kweli, uhakika na uwazi  hakuna mwanachama hata mmoja atakayepoteza haki yake kwa kujiunga na SHIWATA.

Alisema Wanachama waliojiunga na SHIWATA kutoka mwaka 2004 na kufanikiwa kulipa sh. 10,000 za kujiunga na kijiji cha
Mwanzega kupitia mtandao huo na kupatiwa hati wanatakiwa
kufika ofisini Ilala Bungoni na nyaraka zao zote ili
wapelekwe kijijini kukabidhiwa maeneo yao.

Alisema pia wanachama wote waliochangia ujenzi ya nyumba zao kwa kiasi chochote cha fedha kupitia benki wanatakiwa kufika ofisini na nyaraka zao zote ili nao wakakabidhiwe maeneo yao kwa kadri walivyochangia.

Alisema waliochangia katika mgawo wa mashamba katika
shamba la Ngarambe na hatajakabidhiwa mashamba yao
wanatakiwa wafike ofisini na nyaraka zao ili wakakabidhiwe.
 

Taalib alisema wanachama wote wanatakiwa kutekeleza agizo hilo kabla ya Aprili 9, 2015 na kutakuwa na mkutano wa wanachama wote Aprili 10, 2015 ili kupata maelezo zaidi.
 

Alisema SHIWATA ambayo imekamilisha ujenzi wa nyumba 104, tayari wasanii 40 wamejitokeza kuhamia katika kijiji hicho cha Mwanzega, Mkuranga wakiwa huko watajifunza ujasiriamali, na kushiriki katika kilimo cha bustani na pia watatengeneza filamu na tamthilia.

Mwenyekiti huyo alisema kijiji cha wasanii cha Mwanzega,kinaengwa kisasa kifikie kiwango sawa au zaidi ya Nollywood ya Nigeria, Bollywood ya India au Hollywood ya Marekani na tunakusudia kukiita kijiji chetu ni Tallywood.

Alisema kijiji ambacho wanaamini kitakuwa kivutio kikubwa cha utalii na utengenezaji filamu ndani na nje ya nchi ya Tanzania.

mwisho

No comments:

Post a Comment