RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohammed
Shein anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika utoaji wa tuzo za Wanamichezo
Bora Tanzania Ijumaa wiki hii.
Tuzo hizo zinaandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) na mwaka huu zimedhaminiwa na Selcom Wireless, Said Salim Bakhresa & Co Ltd - Bakhresa Group, IPTL, mifuko ya hifadhi ya jamii, PSPF na NSSF.
TASWA
inaishukuru Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa ushirikiano wake na
kukubali Rais Dk. Shein aje katika tuzo zetu, ambazo zitafanyika ukumbi
wa Diamond Jubilee, VIP Dar es Salaam.
Kukubali
kwa Dk. Shein kuwa mgeni rasmi kunaonesha jinsi gani alivyokuwa
mwanamichezo wa kweli na mwenye nia ya dhati ya kushirikiana na wadau wa
michezo nchini.
Katibu
wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo (TASWA) Amir Mhando (kulia)
akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuhusu tuzo za
TASWA zinazotarajiwa kufanyika jumamosi hii katika ukumbi wa Diamond
Jubilee jijini Dar es Salaam. Katikati ni Makamu Mwenyekiti wa TASWA,
Egbert Mkoko na mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Mwani Nyangasa
******************************
******************************
Wanamichezo
44 wanatarajiwa kupewa tuzo siku hiyo baada ya kufanya vizuri katika
michezo mbalimbali kuanzia Juni 2013 hadi Juni 2014. Pia itatolewa Tuzo
ya Mwanamichezo Bora wa jumla na Tuzo ya Heshima.
TASWA
imewahi kutoa Tuzo ya Heshima kwa Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu,
Benjamin Mkapa, pia imewahi kutoa Tuzo ya Heshima kwa timu ya soka ya
Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ iliyokuwa ikicheza mechi za kufuzu
fainali za mataifa ya Afrika mwaka 1980 zilizofanyika Lagos, Nigeria.
Tunaamini
zitakuwa tuzo za aina yake, ambapo tayari Kamati ya Kusimamia Tuzo hizo
imeshatangaza majina ya wanamichezo zaidi ya 100 wanaowania tuzo
mbalimbali.
No comments:
Post a Comment