Dereva Toka Nchini Ujerumani Rainer
Zietlof(katikati)Akizungumza na Wanahabari kuhusiana na rekodi yake ya
kusafiri umbali mrefu Duniani Mara baada ya kuwasili nchini Tanzania
kwenye Ofisi za Alliance Autos,Kulia ni Meneja mkuu wa Alliance Motors
Bwana Wayne Mcintosh na kushoto kwake ni Meneja Masoko wa Alliance Autos Tharaia Ahmed.
******************************************
Na Mwandishi Wetu
DEREVA raia wa Ujerumani Rainer Zietlof yuko mbioni
kuvunja rekodi ya dunia ya kuendesha gari kwa kilometa 17,000 kutoka Ulaya hadi
Afrika.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es
Salaam, Zietlof alisema kuwa hiyo itakuwa ni rekodi yake ya tatu baada ya zile
za awali alizovunja mwaka 2011 na 2012.
Awali alivunja rekodi baada ya safari iliyojulikana
kama `Panamerica’ambayo ilimchukua kutoka Tierra del Fuego hadi Alaska kwa siku
11 na saa 17 wakati ile ya `Russtralia’ ilimtoa Melbourne, Australia hadi St.Petersburg
nchini Urusi ambako alitumia saa 18.
Zietlof anayetumia gari aina ya VW Touareg V6 TDI
alianza rasmi safari yake Septemba 21 mwaka huu huko North Cape nchini Norway
na anatarajia kuikamilisha nchini Afrika Kusini, ambako atakuwa ametembea kwa
kilometa 17,000.
Kwa mujibu wa dereva huyo, safari hiyo ndefu
imempitisha katika nchi za Norway, Finland, Sweden, Denmark, Ujerumani, Jamhuri
ya Czech, Slovakia, Hungary, Serbia, Bulgaria, Uturuki, Misri, Sudan, Ethiopia,
Kenya na sasa Tanzania.
Dereva huyo alizungumza na wandishi wa habari katika
makao makuu ya Alliance Autos iliyopo barabara ya Nyerere jijini Dar es Salaam,
na kusema kuwa atachangia kiasi cha senti
20 za euro kwa kila kilomita, kwa vijiji nchini Tanzania na Zambia.
Mbali na kuahidi kuvichangia vijiji hivyo, Zietlot pia
amesisitiza kuvitembelea vijiji hivyo atakavyo vichangia.
Aidha, amelisifia gari hilo kutokana na uwezo wake wa kukabiliana na
mazingira tofauti tofauti ya hali ya hewa kama baridi kali na joto pamoja na
barabara mbovu.
Mradi huu wa kuzunguka sehemu mbalimbali za dunia kwa
gari hilo umedhaminiwa na makampuni makubwa ya
magari ya Tehama na Volkswagen nchini Ujerumani, Slovakia na Afrika
Kusini.
Katika safari hiyo Zietlow yuko na wasaidizi wake
wawili, Marius Biela ambaye ni mpiga picha na mchukua video huku Matthias Prillwitz
ni mzoefu wa mbio
za magari nchini Ujerumani.
Dereva huyo alianza safari zake za barabarani mwaka
2005 na ameoa na ana mtoto mmoja.
Dereva Toka Nchini Ujerumani Rainer Zietlof(Wa Kwanza Kulia)akiwaelezea jambo wanahabari hawapo pichani Kushoto kwake ni Meneja Masoko wa Alliance Autos Tharaia Ahmed
Meneja mkuu wa Alliance Motors Bwana Wayne
Mcintosh akielezea ni kwa namna gani magari yao yako imara kuhimili
masafa marefu akitolea gari ya Volsk Wagen Aliyosafiri nayo Dereva Toka
Nchini Ujerumani Rainer Zietlof
Dereva Toka Nchini Ujerumani Rainer Zietlof akioyesha cheti cha rekodi ya dunia mbele ya wanahabari
Dereva Toka Nchini Ujerumani Rainer Zietlof akitoa maelekezo ya gari yake aina ya Volkswagen Touareg V6 TDI
Dereva Toka Nchini Ujerumani Rainer Zietlof akitoa maelekezo ya injini ya gari yake aina ya Volkswagen Touareg V6 TDI aliyosafiri nayo kwenye nchi zaidi ya 19 Duniani
Dereva Toka Nchini Ujerumani Rainer Zietlof akitoa maelekezo ya bodi ya gari yake aina ya Volkswagen Touareg V6 TDI aliyosafiri nayo kwenye nchi zaidi ya 19 Duniani
Dereva Toka Nchini Ujerumani Rainer Zietlof akitoa maelekezo ya sehemu ya kuweka vifaa vya akiba kwenye gari yake aina ya Volkswagen Touareg V6 TDI
Dereva Toka Nchini Ujerumani Rainer Zietlof akiendelea kutoa maelekezo ya Gari yake hiyo aina ya Volkswagen Touareg V6 TDI
Gari aina ya Volkswagen Touareg V6 TDI inavyoonekana kwa ndani
Dereva Toka Nchini Ujerumani Rainer Zietlof akiwa na Meneja mkuu wa Alliance Autos Bwana Wayne Mcintosh(wa pili toka kulia)wakipata picha ya pamoja na wanahabari
No comments:
Post a Comment