BINGWA wa mwaka huu katika mashindano ya Kombe la OG Wala Wala aazawadiwa seti mbili za jezi, mipira mitatu na sh. 100,000 taslim na mshindi wa pili atapata zawadi kama hiyo lakini atapata jezi seti moja na mpira miwili.
Msemaji wa Kombe la Wala Wala, Yusufu Shemweta maarufu kama Majisafi alisema jana kuwa kila kundi kati ya mawili ya inaingiza timu nne katika Robo fainali inayotarajiwa kuwa na mvutano ya hali ya juu.
Timu nane kati ya 18 zinazoshiriki mashindano ya Kombe la OG Wala Wala yanayofanyika kwenye uwanja wa Jitegemee mjini Muheza Jumatano Septemba 18 zinaingia kwenye robo fainali ya kumpata bingwa wamwaka huu.
Shemweta ambaye pia ni Mwenyekiti wa Shirikisho la Soka Wilaya ya Muheza (TFF) alisema mshindi wa tatu atazawadiwajezi seti moja, mpira mmoja nafedhataslimu sh. 100,000 na timunyingine zilizoshiriki mashindano hayo zitazawadiwa mpira mmoja nafedhash. 100,000.
Alizitajatimu zinazoshiriki mashindano hayo kutoka kundi A ni Kilimo FC, Mkumbi FC, Chipukizi FC, Uruguay FC, Mafundi FC, Miembeni, Muheza United, Lusanga Star na Black Fighter.
Kutoka kundi B kuna timu za Tax Driver FC, Wabambino FC, Mkanyageni FC, Shoeshine FC, Kwamkadala FC , Magila Star, Wakosanamba FC, Kwa Mkangala FC na Kitisa FC.
mwisho
No comments:
Post a Comment