Pichani
ni baadhi ya wateja wakipata maelezo maelezo mbalimbali kuhusiana na
huduma zitolewazao na Kampuni ya simu TTCL,ndani ya banda la kampuni
hiyo ndani ya maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea hivi
sasa jijini Dar Es Salaam.
Wahudumu
wa TTCL wakihudumia wateja wao kwa njia ya simu ndani ya banda
lao,katika maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea hivi
sasa jijini Dar Es Salaam.
Namna mkongo wa Taifa unavyofanya kazi na maeneo mbalimbali ulivyosambaa nchini
Afisa
Biashara Mkongo wa Taifa wa mawasiliano,Bwa.Thomas Lemunge akielezea
kuhusiana na Mkongo wa Taifa wa mawasiliano unavyofanya kazi mapema leo
ndani ya maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea hivi sasa jijini Dar Es Salaam.
Bwa.Thomas
amebainisha kuwa Mkongo wa Taifa wa mawasiliano umekwisha sambaa maeneo
mengi ikiwemo mikoa 21 ya Tanzania mpaka sasa,Amesema kuwa Makampuni
yote ya ndani yanatumia mkongo huu wa mawasiliano kupeleka huduma kwa
wananchi na kuongeza kuwa Mkongo huo unaunganisha mataifa mbalimbali
kupitia mkongo huu wa Taifa wa Mawasiliano ambao umerahisisha mambo
mengi katika jamii ikiwemo suala zima la mawasialiano ya simu za
kiganjani na mambo mengineyo.
Bwa.Thomasa
amewataka wananchi kuhakikisha wanautunza na kuulinda Mkongo huo wa
mawasiliano ili kuendelea kurahusisha upatikanaji wa huduma mbalimbali.
Baadhi ya Wahudumu wa kampuni ya simu ya TTCL wakiendelea kuwajibika.
Afisa
Mahusiano wa kampuni ya Simu ya TTCL-Tanzania,Bwa.Edwini Mashashi
akielezea kuhusiana na huduma zao mbalimbali zitolewazo na kampuni
hiyo,ikiwemo masuala ya Internet na huduma nyinginezo mbalimbali kwa
wateja wao.
Bwa.Edwin
ameeleza kuwa kwa sasa kampuni yao iko katika mchakato mkubwa wa
kuziboresha huduma zao ziwe na ubora zaidi,ameongeza kusema kuwa pia
Wanatarajia kufunga Wi-Fi katika maeneo mbalimbalu ya jiji la Dar,
ambapo gharama itakuwa ni ya bei nafuu.
Edwin
amesema kuwa Kampuni ya TTCl-Tanzania,wanatarajia kuzindua kituo
kikubwa Afrika Mashariki cha kuuzia internet,kituo hicho kinatarajia
kuzinduliwa mwishoni mwa mwezi Julai ama Agosti,''mtambo huo tayari
umekwishafungwa hapa hapa nchini tayari kwa kuanza kutoa huduma hiyo
Afrika Mashariki,hivyo kutakuwa hakuna haja tena ya kununua tena
Internet nje'',amedema Bwa.Edwin
No comments:
Post a Comment