TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION

TANGAZO SHIWATA

Sunday 29 June 2014

UCHAGUZI SIMBA NGOMA INOGILE

Na Mwandishi Wetu

KAMA uchaguzi mbovu uliowahi kufanyika katika klabu ya Simba kutoka miaka ya sabini uchaguzi huu wa mwaka 2014 ambao Mwenyekiti anayemaliza muda wake Ismail Adena Rage hakugombea ulichelewa kuanza na utaratibu wa kupiga kura ulitoa mwanya kwa wanachama wasioitakia mema Klabu hiyo kupiga kura mara mbili hadi tatu.

Msimamizi wa uchaguzi, Amin Bakhresa hakuwa makini kusimamia ipasavyo umati mkubwa wa wanachama wa Simba waliojitokeza kwenye ukumbi wa Polisi Oficers Mess kupiga kura ya kumchagua Rais, Makamu, na wajumbe watano wa Kamati ya Utendaji ambapo mmoja wao ni mwanamke.

Kila mwanachama alipewa kura zote na apige kura kwa wakati mmoja lakini kutokana na kutokuwa na umakini waliopiga kura mara ya kwanza walirudia tena na hivyo kuashiria wapiga kura kuwa wachache lakini kura za kuwachagua viongozi kuwa nyingi.

Mpaka saa 12 jioni matokeo bado yalikuwa yakihesabiwa na wagombea wote wakiwa katika wakati mgumu kujua hatma yao kama wamepata nafasi ya kuiongoza Simba hii ambayo imeamua kurejesha hadhi yake ama wametupwa nje ya ulingo.

Wanachama kutoka mikoa ya jirani baada ya kupiga kura waliondoka na kubaki wanachama wachache kutoka matawi ya Dar es Salaam ambao walikuwa na shauku ya kujua nani ni nani kapata nafasi ya kuwa kiongozi katika klabu ya Simba.

mwisho

No comments:

Post a Comment