TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION

TANGAZO SHIWATA

Thursday, 22 May 2014

Warembo, wadhamini watakiwa Miss Sinza



 Miss Sinza 2013 Prisca Clement katikati mara baada ya kushinda taji la vipaji katika mashindano ya Miss Tanzania 2013
=======  ======  ======
Waandaaji wa mashindano ya kumsaka mrembo wa Sinza, Miss 2014 wametoa wito kwa wasichana wenye vigezo vya kuwania taji la mwaka huu kujitokeza katika mazoezi yanayoendelea kwenye ukumbi wa Meeda Club uliopo katika barabara ya Sinza Mori na Lufungila jijini.

Akizungumza jijini jana, Muandaaji wa mashindano hayo, Majuto Omary alisema kuwa lengo lao ni kuwa na warembo wengi ili kuwapa nafasi majaji kuchagua washindi ambao wataiwakilisha vyema Sinza na vitongoji vyake katika mashindano ya Kanda ya Kinondoni na Miss Tanzania.

Majuto alisema kuwa mpaka sasa jumla ya warembo nane wamejitokeza katika mazoezi ya mwaka huu, idadi ambao haitoshi kutokana na malengo yao ambayo ni warembo 20.

Alisema kuwa uwepo wa washindani wengi, kunatoa changamoto hata kwa majaji na kutoa mrembo bora zaidi na kuwa mwakilishi wa kweli. “Hatujafunga milango ya kuwapokea warembo, tunawaomba wafike mazoezini kuanzia saa 10.30 jioni na kukutana na wakufunzi wetu, Fomu  zinatolewa bure,” alisema Majuto. Majuto pia aliwaomba wadau wa mashindano ya urembo nchini kujitokeza kudhamini mashindano hayo kwa lengo la kuleta maendeleo, kuongeza ushindano mbali ya kutangaza biashara zao.

Alisema kuwa ni fursa pekee kudhamini mashindano hayo kutokana na mvuto uliopo, kwani watazamaji wengi ufika kuangalia mazoezi na wakati wa mashindano.

Taji la Miss Sinza linashikiliwa na Miss Tanzania, Prisca Clement alimaliza katika hatua ya 10 bora katika mashindano ya mwaka jana ya Miss Tanzania na pia alishinda taji la mrembo mwenye kipaji katika mashindano hayo.

No comments:

Post a Comment