Rais
wa Shirikisho la Muziki Tanzania, Addo Novemba, akizungumza jambo
katika kikao cha wadau wa muziki juu ya ujio wa mwili wa marehemu Amina
Ngaluma, anayeletwa kesho usiku ukitokea nchini Thailand, alipofia.
Anayefuata ni mume wa marehemu, Rashid Sumuni, Mwinjuma Muumini na Said
Mdoe aliyeshika kidevu.
Katika
kikao hicho, Rais wa Bongo Movie, Steve Nyerere alionyesha kuchukizwa
vikali na ujio mdogo wa wadau wa muziki kujadili kuletwa kwa marehemu.
Steve aliwataka waimbaji na wasanii wote kuwa makini pamoja na
kushirikiana wao kwa wao ili wajiwekee mazingira mazuri.
Katika
kikao hicho, ilitangazwa kuwa jumla ya shilingi milioni tano
zinahitajika kufanikisha mazishi ya mkali huyo nchini, akikumbukwa sana
na wimbo wake Mgumba namba 2, akiwa ndani ya Double M Sound, chini ya
Mwinjuma Muumini.
Rais
wa Bongo Movie Tanzania, Steve Nyerere akichangia hoja katika kikao
hicho cha kujadili msiba huo, ambapo jumla ya shilingi milioni tano
zinahitajika ili kuhakikisha kuwa mwili wa Amina unawasili na kuzikwa
kama inavyostahiki.
Miongoni
mwa wadau waliojitokeza katika kikao hicho wakisikiliza kwa umakini juu
ya kikao cha wadau wa muziki wa dansi juu ya msiba wa Amina Ngaluma.
Kikao hicho kilifanyika leo saa tano asubuhi katika Ukumbi wa Vijana
Social Hall, Kinondoni, jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment