Na Peter Mwenda
MVUA za Masika
zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam zimewafanya baadhi ya wazazi
kuwazuia watoto wao kwenda shule kuhofia kuzama kwenye madaraja
yaliyozolewa kulikosababisha magari kushindwa kupita.Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Abuu Jumaa ya Kivule DAr es Salaam , Floida Nkya akizungumza jana alisema kutoka mvua zianze mahudhurio katika shule yake imekuwa hafifu aliwahoji kujua tatizo aliambiwa wazazi wao hawako tayari kuwaruhusu watoto wao kupoteza maisha kwa kuzama maji baada ya madaraja kubomoka.
Mmoja wa wazazi wa wanafunzi wanaosoma shule hiyo, John Roko alisema wanafunzi wanaosoma shule ya Abuu Jumaa,Shule ya Sekondari Kivule na Shule ya Msingi KIvule hawafiki shuleni kutokana na kuharibika kwa barabara kunakosababisha usafiri kuwa mgumu kwa sababu mabasi ya abiria hayaendi njia hiyo.
Bw. Roko aliomba Serikali kufanya jitihada za haraka
kunusuru hali ngumu ya usafiri katika baadhi ya maeneo ya Kata ya Kivule
ambayo hayafikiki kabisa kutokana navivuko kuzolewa na mvua na
kuwatenganisha wananchi wa sehemu moja hadi nyingine.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kivule, Joseph Gassaya
alipoulizwa kuhusu hali hiyo alisema jitihada zinafanyika za kukarabati
madaraja na vivuko vilivyozolewa na maji na pia kwa nguvu za wananchi
wamejitahidi kujenga madaraja ya muda ili ianze kupitika wakati
inasuburi Manispaa ya Ilala na Serikali Kuu kunusuru hali hiyo.
mwisho
No comments:
Post a Comment