KHALID CHOKORAA KUPANDA ULINGONI MAY 24 KUZIPIGA NA ABDUL MANYENZA
Mwanamuziki
na kiongozi wa bendi ya Mapacha watatu Khalid chokoraa anategemea
kupanda ulingoni jumamosi ya tarehe 24 katika ukumbi wa friends corner kuzipiga na bondia chipukizi mwenye uchu wa ushindi muda wote awpo ulingoni Abdul manyenza. Chokoraa alisema muda mrefu amekuwa akifanya mazoezi ya kujenga
mwili na ya ngumi kwa muda mrefu na amekuwa akipigana na mabondia
tofautitofauti mazoezini na kuona uwezo wao ni wa kawaida, hivyo anataka
kuwaonesha kama ana kipaji kingine zaidi ya kuimbia, kwa sasa amekuwa akijifua katika gym ya bigright boxing ya mwananyamala chini ya mwalimu wake bondia mkongwe
omar athuman ‘van dame’ kwa lengo la kumsambaratisha mpinzani wake
ambae amekuwa akijitapa kumfukuza chokoraaa kwa kipondo kikali arudi
kuimba. Siku hiyo ya jumamosi kutakuwa na mapambano ya ubingwa kati ya
Karama nyilawila na Said Mbelwa wakigombea
ubingwa wa UBO-AFRICA ,wakisindikizwa na kina chokoraa na Abdul
manyenza, Suleiman Galile akimkabili Abdala Pazi ‘kiroba’ nae bingwa
wa afrika Alan kamote wataoneshana umwamba na Adam ngange, Ramadhan
kumbele atazipiga na Hassan kiwale”morobest” , idd athuman na julias
kisarawe, nao wababe wa majigambo Zumba kukwe wataoneshana kazi na
Kamanda wa makamanda, pia kutakuwa na pambano mengine mengi tu ya
utangulizi ya mabondia wa tanga watazipiga na mabondia wa dare es
salaam. Kama vile Athuman boxa wa tanga atazipiga na waite juma wa
chalinze, Rajabu mahoja wa tanga atazipiga na kaisi wa darn a mengineyo
yenye kuleta hamasa na burudani za mchezo wa ngumi, kwa vijana kuonesha
vipaji vyao
No comments:
Post a Comment