TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION

TANGAZO SHIWATA

Wednesday, 9 April 2014

TIMU YA WATOTO WA MTAANI WALIOCHUKUA UBINGWA BRAZIL WATUA NCHINI NA KOMBE


Viongozi wa timu ya watoto wa mitaani wakiwa na vikombe walivyonyakuwa wakiwa jijini Rio de Janeiro, Brazil baada ya kutua katika
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 9 na nusu jioni kwa ndege ya Emirates' jana Picha na Rajabu Mhamila

''Tunaipongeza timu ya Tanzania ya Watoto wa Mitaani kwa kutwaa ubingwa wa Dunia wa Watoto wa Mitaani baada ya majuzi (Aprili 6 mwaka huu) kuifunga Burundi mabao 3-1 katika mchezo wa fainali uliochezwa jijini Rio de Janeiro, Brazil.

Ushindi kwa timu hiyo ni fahari kwa Tanzania, lakini kubwa ni kwa kituo cha Mwanza ambacho ndicho kinachoiendesha pamoja na wadhamini na wafadhili walioiwezesha kushiriki fainali hizo kwa mara ya pili mfululizo.

Vilevile ushindi huo unatoa changamoto kubwa kwa wadau wa mpira wa miguu kuwa watoto wa mitaani ni sehemu tu ya vipaji vilivyotapaa nchini, hivyo iliyopo ni kuvisaka na kuvibaini vipaji hivyo kwa ajili ya ustawi wa mchezo huo nchini.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) tutaendelea kushirikiana na kituo hicho cha Mwanza, na vingine vyote ambavyo vinajishughulisha na mchezo huu, lengo likiwa ni kuundeleza na hata kutoa ajira kwa vijana hapo baadaye kupitia mpira wa miguu.


Timu hiyo imerejea nchini leo ambapo imetua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 9 na nusu jioni kwa ndege ya Emirates''

No comments:

Post a Comment