TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION

TANGAZO SHIWATA

Tuesday 15 April 2014

SEIF SHARIFF HAMAD KAZUNGUMZA LEO, KAULI ZAKE 7 KUHUSU MUUNGANO ZIKO HAPA



Maalim Seif Sharif Hamad.
Amekua mmiliki wa vichwa vya habari kutokana na ripoti mbalimbali ambazo zimekua zikimnukuu kwa kudai kutoutaka muungano lakini leo April 15 2014 amezungumza kwenye maonyesho ya miaka 50 ya muungano ya kuzitoa hizi kauli zifuatazo.
1. ‘Pamoja na milima na mabonde, muungano huu umedumu miaka 50, nchi nyingine zilishindwa, lazima tufanye tathmini hasa ya muungano wetu, lazima vijana waelimishwe vp muungano uliundwa, tulianzia vipi’
2.‘Ukitaka upate maenedeleo, yatambue mafanikio yako lakini pia usisahau matatizo yako, ni ni moja.. kufanya vizuri, Sidhani katika Tanzania kama kuna watu hawataki muungano, na kama wapo ni wachache, muungano uendelee ndio la msingi’
3. ‘Sio dhambi watu kuwa na fikra tofauti, sio dhambi hata kidogo kwa sababu hatuwezi wote kuwa na fikra aina moja, Wanaotaka serikali moja wasibezwe, mbili wasibezwe, wanaotaka tatu na serikali ya mkataba wasikilizwe pia’
4. ‘Wako wanaoamini kwamba matatizo ya muungano yako kwenye muundo, tuwasikilize wana hoja gani, Mwaka 1963 Malaysia na Tanganyika maendeleo ya sehemu zote hizi yalikua sawa, mwaka 2014 tujiulize, changamoto kwetu ni vipi tutakua na muungano utakaokua ni chachu ya maendeleo ya haraka, mambo ya 74 ni tofauti na 2014′
5. ‘Tuwe makini sana, sote ni wa nchi moja, tujiepushe na kikundi chochote kuona wao wana haki zaidi, Watanzania wote sawa, wajumbe wa bunge maalum waangalie maslahi ya nchi, muungano huu ni wa nchi 2 zilizokua dola huru na kuungana kwa hiari’
6. ‘Tupate katiba ambayo itaondoa migogoro, kero iwe ni historia… hili swala lisiwepo tena, tusiende kwenye maamuzi ya harahaharaka tukasema serikali mbili au tatu bila kuangalia athari zake, katiba ya Znz inasema ni miongoni mwa nchi mbili za muungano, ya Muungano inasema Tz ni nchi moja, huo ni mgogoro’
7. ‘Nadhani Warioba walivyopendekezwa waliona hisia za Znz zilivyo, tunataka katiba itakayotambua usawa wa nchi mbili, hakuwezi kuwa na katiba ambayo itamridhisha kila mtu lakini angalau wengi wao waridhike’
CHANZO NI MILLARDAYO.COM

No comments:

Post a Comment