TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION

TANGAZO SHIWATA

Thursday, 10 April 2014

MARUFUKU BODA BODA NA BAJAJI ZA ABIRIA KUVUKA MWENGE KWENDA POSTA.



Oparesheni Nzito ya kuzuia Bodaboda na Bajaji zisifanye safari zake  kutoka Mwenge na maeneo mengine kuelekea mjini Posta imechukua sura mpya leo baada ya Askari wa Usalama wa Barabarani kuanza kukamata Bodaboda na Bajaji zote zinazovuka Mwenge kuelekea Posta, Zoezi hilo ambalo limefanyika Mwenge Mataa Jijini Dar limeendelea kufanyika na kufamikiwa kuwanasa wengi.
Kwa mujibu wa Msemaji na Muongozaji wa Oparesheni hiyo ambaye hakutaka kutajwa jina lake alisema kwamba wameamua kufanya hivyo ili kuzuia Msongamano wa Magari pamoja na bodaboda pia Bajaji kuelekea Mjini Posta, Aliongeza kuwa kumekuwa na uhalifu sana wa Silaha unaotumiwa na bodaboda hasa maeneo ya mjini hivyo ndio maana wameamua kuzuia.
"Tumefanya hivi ili kuepusha msongamano kuelekea Posta, lakini pia kumekuwa na uhalifu sana unaotumiwa kwa njia ya Bodaboda hivyo tunafanya oparesheni hii ili kupunguza tatizo hili. Tulicho kifanya tumewaruhusu kufanya safari pembezoni mwa mji tuu hivyo Eneo la Mwenge kwa sasa Limeingia katika zone ya eneo la Mjini,Kama tuliweza kuzuia Daladala ndogo"Hiace" pia na hawa watakuja kuelewa ingawa ni zoezi gumu na linalo hitaji elimu ya ziada ambayo tumesha anza kuwapa na tunaendelea kuwapa"  alimalizia kwa kusema "Pia hii ni Oparesheni ya kawaida tuu ya kukamata wale ambao hawana Leseni za kuendesha vyombo hivi pamoja na makosa mbalimbali" alisema Polisi huyo.

Kwa mujibu wa madereva wa Bodaboda na Bajaji wamesema kwamba huo ni uonevu kuwakataza wao wasiweze kwenda Mjini kwani na wao wanatafuta ridhiki yao na wameomba Serikali iwasaidie wapatiwe njia mbadala ya wao kwenda maeneo hayo. 

Wanao ruhusiwa kwenda Posta na Bajaji au Bodaboda ni wale ambao ni wamiliki binafsi na wanatakiwa wapite njia hizo wakiwa Bila abiria yoyote.
 Oparesheni Kamata Bodaboda na Bajaji ikiwa inaendelea upande wa Mwenge mataa ambapo Bajaji nyingi zimekamatwa
 Askari wa Usalama wa Barabarani akiwa anawaandikisha Baadhi ya Bodaboda na Bajaji wenye makosa mbalimbali ili waweze kulipia tozo pamoja na kupelekwa kituo cha Polisi.
 Baadhi ya Bodaboda na Bajaji wakiwa wanangojea Hatma yao baada ya kukamatwa
 Huu ni upande wa kutokea Mwenge kuelekea Posta ambapo Bajaji haziruhusiwi kuvuka hapo kuelekea Posta
 Baadhi ya Madereva wa Bajaji na Boda boda wakijadiliana Juu ya swala hilo la kuzuiliwa kuelekea Posta

 Baadhi ya Bodaboda zikiwa zimekamatwa
  Madereva wa Boda Boda na Bajaji wakipata maelezo ya kina ya kwanini wamezuiliwa  kwenda Posta wakitokea Mwenge
 Mmoja wa Madereva wa Bodaboda akiwa amekaa kwa Mawazo asijue anafanya nini Baada ya Bodaboda yake kukamatwa na Kupelekwa Polisi.

Picha na Dar es salaam yetu

No comments:

Post a Comment