TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION

TANGAZO SHIWATA

Tuesday, 29 April 2014

Kamanda Kova afunguka vifo vya watoto Bwawa la Kuogolea Dar




Picha haihusiani na habari, ila watoto wakifurahia kuoga kwenye bwawa la kuogolea kama wanavyuoonekana
KAMANDA wa Polisi Kanda Maalum  Suleiman Kova amefafanua juu ya taarifa ya vifo vya watoto watatu
waliofariki wakati wakiongolea kwenye bwawa la hoteli.
Kamanda Kova alisema April 27  kulitokea vifo vya watoto 3 ambao walikua na birthday party nyumbani lakini baada ya kukamilika kwa taratibu za party ya nyumbani waliamua kuimalizia party hiyo hotel ya Landmark,walipofika walienda kuogelea kwenye swimming pool ya watoto lakini baadae watoto hao walitoka kwenye pool ile ya watoto wakaingia kwenye pool ya wakubwa na kwa bahati mbaya waliingia sehemu yenye kina kirefu.
Watoto wenzao walipoona wenzao wanazama walianza kuwavuta kuwatoa nje lakini hali zao tayari zilikua mbaya, mmoja wapo hali yake ilikua kidogo afadhari lakini kwa bahati mbaya nayeye alifia hospital wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya Masana na kufanya Idadi ya watoto waliofariki kuwa 3 majina yao ni Janet Zacharia, Eva na Ndimbuni.
Kamanda Kova amesema; "’Kusema kweli sio mara ya kwanza kutokea, mara nyingi vifo vya watoto vinatokana na uangalifu au uzembe kutoka kwa wale wanaotakiwa kuwaangalia hao watoto wao, hizi hotel zote zenye swimming pool lile eneo la kuogelewa basi wasiruhusiwe watoto wadogo kuogelea au kuwe na mtu ambaye anajua kuogelea au kuokoa ambaye yupo pale’
‘Unajua watoto wana tabia ya kuigana mmoja akiingia akiogelea pengine anafahamu kidogo wengine wote wanafata mkumbo wanaona wanaweza,sisi kama jeshi la Polisi tumeamua hili kosa la uzembe kusababaisha kifo kisheria mtu anaweza kushtakiwa kwa kuzembea kwa kutochukua tahadhari mpaka watoto kama wale ambao hawana hatia uwezo wao mdogo wa kufikiri au kuijiokoa’
‘Tunafatilia kwa umakini lakini jukumu la kufatilia maisha ya watoto ni la wazazi mia kwa mia wasipofanya hivi wakiwa hawapo makini matokeo yake ni haya watoto 3 wamefariki,tunaendelea na uchunguzi na baadae tutatoa taarifa kamili’.

No comments:

Post a Comment