Afisa uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde (kushoto) akimkabithi mfano wa hundimwenyekiti
na Mratibu wa Mradi wa The Unity of Women friends Maryam Shamo wakati
wa halfa ya Tuzo za Mwanamakuka 2014 ambapo Airtel Tanzania ni moja kati
ya Wadhamini wa tuzo hizo, Bi Leil Mwambungu aliibuka na kutangazwa
mshindi wa mwanamakuka 2014. Akishuhudia ni Mkurugenzi Mkuu wa Bank ya
Wanawake Tanzania Bi Margreth Chacha (wakwanza kulia), Hafla ya
mwanamakuka ilifanyika jana katika ukumbi wa Escape 1 mikocheni Dar es
salaam.
Afisa
uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde (kulia) akimpongeza mshindi wa
mwanamakuka 2014 bi Leila Mwambungu mara baada ya kutangazwa katika
halfa ya Tuzo za mwanamakuka iliyofanyika Escape 1 jijini Dar esaalam
mshindi wa mwanamakuka
2014 bi Leila Mwambungu mara baada ya kutangazwa katika hafla ya Tuzo za
mwanamakuka iliyofanyika Escape 1 jijini Dar esaalam, pichani kushoto
ni Mkurugenzi Mkuu wa Bank ya Wanawake Tanzania Bi Margreth Chacha
======== ======== =========
Kampuni
ya simu za mkononi ya Airtel imekabithi waandaaji wa Tuzo za
mwanamakuka The Unity of Women Friends kiasi cha million tano pesa
taslimu wakati wa halfa ya tuzo za mwanamakuka 2014 zilizofanyika
jijini Dar es saalam mwisho wa wiki
Tuzo
hizi za mwanamakuka 2014 ziliwashirikiasha washindi 10 wa mwaka 2012 na
mwaka 2013 ambapo washindi hawa walifatiliwa biashara zao na
kuchaguliwa mshindi mmoja aliyefanya vizuri na kutumia vyema zawadi
aliyoshinda katika kuendeleza biashara zao ambapo bi Leila Mwambungu
aliyekuwa mshindi wa pili mwaka Jana kuibuka kuwa mshindi wa mwanamakuka
2014
Akiongea
wakati wa kukabithi zawadi hiyo, Afisa Uhusiano wa Airtel bi Jane
Matinde alisema” Tunayofuraha kuwa wadhamini wa tuzo hizi za
mwanamakuka kwa miaka mitatu mfululizo kwa sasa na kuwa sehemu ya kuleta
mabadiliko kwa wanawake kupitia tuzo hizi. tunafurahi kuona jinsi kina
mama hawa wajasiriamali walioshinda miaka iliyopita wakifanya vizuri
katika biashara zao.
Na
sisi Airtel leo tunakabithi kiasi cha kiasi cha shilingi milioni tano
kama mchango wetu kwa tuzo hizi za mwanamakuka kwa mwaka 2014. Tunaamini
kiasi hichi cha fedha kitaweza kuwawezesha waaandawaji wa tuzo hizi
kufanikisha halfa hii na kuwafikia wanawake na kuwawezesha kutanua
mitaji yao na hatimae kuongeza kipato na faida zaidi na kujikwamua
kiuchumi”.
“Tutaendelea
kushirikiana na The unity of Women Friends ili kuhakikisha tunaweza
kuwafikia wanawake wengi zaidi nchini” aliongeza Matinde.
Kwa
upande wake mshindi wa mwanamakuka 2014 bi Leila Mwambungu Alisema
“naona fahari na furaha kuwa mshindi wa tuzo hizi za mwanamakuka kwa
mwaka huu, napenda kuwashukuru sana waandaaji wa tuzo hizi kwa kuniona
kupitia juhudi ninazoziweka katika kazi zangu na biashara zangu. Mpaka
sasa nimeweza kuajiri watanzania kupitia biashara zangu na Kiasi hii
nilichozawadiwa leo kitanisaidia sana kukuza mtaji.
Cha msingi wanawake tupendane na kushirikiana napenda kuwahasa wanawake wenzangu kutokata tamaa na kuongeza katika biashara zao, haijalishi kama mtaji mdogo bali wajipange na kujikita katika uzalishaji na hatimae kuinua mtaji na kuweza kufanya biasha kwa mtaji mkubwa, hakuna siri nyingine ya mafanikio zaidi ya jitihada , hari na kujiwekea malengo na kuhakikisha yanafikiwa kwa wakati uliopagwa.
Cha msingi wanawake tupendane na kushirikiana napenda kuwahasa wanawake wenzangu kutokata tamaa na kuongeza katika biashara zao, haijalishi kama mtaji mdogo bali wajipange na kujikita katika uzalishaji na hatimae kuinua mtaji na kuweza kufanya biasha kwa mtaji mkubwa, hakuna siri nyingine ya mafanikio zaidi ya jitihada , hari na kujiwekea malengo na kuhakikisha yanafikiwa kwa wakati uliopagwa.
Naye
mwenyekiti na Mratibu wa Mradi wa The Unity of Women friends Maryam
Shamo alisema Tuzo hizi za Mwanamakuka zinaendelea kukua na kuziboresha
zaidi, kwa mwaka huu lengo letu lilikuwa ni kuwawezesha wachache kwa
kuwafatilia washindi wetu 10 wamiaka iliyopita na kuona jinsi gani
biashara zao zinavyoenda na kumzawadia anayefanya vizuri zaidi. Lengo ni
kuendelea kuwahamasisha na kufatilia mafanikio yao kwa karibu.
vilevule
tukiangalia miaka iliyopita tuliweza kuwashirikisha wanawake tu katika
sherehe za tuzo hizi lakini kwa mwaka huu tumeamua kushirikisha familia
kwa kuandaa bonanza ambapo wakinababa na watoto kwa pamoja
tunasherehekea mafanikio haya, na kusherehekea siku ya wanawake duaniani
huku tukienzi juhudi za wanawake jasiri nchini na kuwazawadia
Tunashukuru
sana Airtel kwa kushirikiana nasi miaka mitatu kwa sasa na tunaamini
kuwa bado wataendelea kutoa mchango wao na kushirikiana nasi na kutuunga
mkono kwa miaka mengine ijayo na kuhakikisha lengo letu la kumwinua
mwanamke wa kitanzania linafikiwa. Alisema Shamo
Kwa
mwaka huu Tuzo hizi zilishirikisha washindi waliopatikana miaka
iliyopita ambapo kati yao pamoja na Tatu Ngao, Mwananne Msekalile,
Sikudhani Daudi, Nasra, Aziz, Khalid, Leila Mwambungu, Selestina
Renatus, Maajab Yusufu na Agnes Daudi ambapo Bi Leila Mwambungu Ameibuka kuwa mshindi wa mwanamakuka 2014
No comments:
Post a Comment