WAANDISHI WA HABARI WASUSIA MKUTANO WA JUMA NKAMIA OFISINI YAKE MPYA,SOMA ZAIDI.
Na Mwandhishi Wetu
SIKU moja kupita baada ya Rais Jakaya Kikwete kuwapisha Baraza jipya la mawaziri, Naibu Waziri mpya wa Habari na michezo, Juma Nkamia ameonja Joto la Jiwe baada ya kususiwa na Waandishi wa habari wa vyombo binafsi pamoja mashirika ya dini.
Taarifa ambazo Mwandishi wa mtandao huu amezipata kutoka ndani ya Wizara ya hiyo ya Habari zinasema tukio hilo lilitokea wakati, Naibu huyo alipokuwa anakabidhiwa ofisi za Wizara hiyo ili kuanza kazi,
Chanzo hicho kinasema, Chombo kimoja cha habari tu ndio kiliwepo ambacho chombo kinatoka Shirika la Utangazaji nchini TBC One.
Uchanguzi uliofanywa na mwandishi wa mtandao huu unasema kitendo cha waandishi kususia mkutano huo ni kutokana na mazimio yaliyotolewa na Wamiliki wa Vyombo vya Habari Nchini (MOAT) Kutoandika habari zozote zinazomuhusu Waziri wa Habari Dkt. Fenella Mukangara pamoja na
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo) kutokana na kufungiwa magazeti ya Mtanzania pamoja gazeti la Mwananchi,huwenda ikawasababu.
Vilevile Sababu nyingine iliyotajwa ni wakati mbunge huyo wa Kondoa Kusini, wakati anachangia bajeti ya Wizara ya Habari na Michezo kwa mwaka 2013-2014 aliwaonesha dharau kwa Baraza la Habari nchini (MCT) kwa kusema Chombo hicho ni “NGOs”na wala hakiko kwa ajili ya kumsimamia waandishi wa habari nchini huwenda ikawa sababu
No comments:
Post a Comment