| Balozi wa kampeni za Usalama barabarani, Bw. Athumani Hamisi akizungumzia athari zinazotokana na ajali za barabarani na kuwaasa wananchi waziepuke hususani katika msimu huu wa sikukuu. |
Airtel , Baraza la Usalama Barabarani kuhamasisha Usalama barabarani msimu wa sikukuu
· Watanzania waaswa kutumia huduma ya bure ya Airtel Money kutuma na kutoa pesa
Dar es Salaam, Disemba 23, 2013 Kampuni
ya mitandao wa simu za mkononi ya Airtel Tanzania imeendeleza
ushirikiano wake na Baraza la Taifa la Usalama barabarani katika juhudi
za kuelimisha uma kuzingatia sheria na kanuni za usalama barabarani
hususani msimu huu wa sikukuu.
Airtel
imekuwa ikishirikiana kwa karibu na kikosi cha Usalama Barabarani
katika kutoa elimu ya usalama barabarani kwa kudhamini kampeni
mbalimbali.
Akizungumza
kwa niaba ya Kampuni hiyo, Meneja wa huduma za kijamii wa Airtel
Tanzania, Hawa Bayumi alisema kipindi hiki cha mwisho wa mwaka wananchi
wanapaswa kuwa waangalifu zaidi ili kujikinga na ajali za barabarani.
“Hiki
ni kipindi ambacho wananchi wanapaswa kuwa makini sana katika
kuhakikisha wanajilinda na wimbi la ajali za barabarani ambazo
husababisha asara kubwa kwa taifa, na pia madereva wajitaidi sana
kuepuka ulevi wa kupindukia,” alisema Hawa.
Aliongeza
kwa kusema pia katika msimu huu wateja wa Airtel wanaweza kutumia
huduma ya Airtel money kutuma na kupokea pesa bure mahali popote nchi
nzima kuepuka kutembea na viwango vikubwa vya pesa.
Kwa
upande wake Katibu Mtendaji wa Baraza na Kamanda wa Kikosi cha Usalama
Barabarani cha Tanzania, DCP Mohammed Mpinga alisema Lengo la kampeni
hizi ni kupunguza ongezeko la ajali za barabarani pamoja na madhara yake
kwa kipindi cha sikukuu za mwaka huu 2013/2014 na wanajitaidi
kuhakikisha elimu inatolewa ipasavyo.
“Tunashukuru
Airtel kwa kuungana nasi katika kujali usalama wa watanzania, kazi ya
kuelimisha watumiaji wa barabara ni kubwa na hivyo tunaendelea kutoa
wito kwa wadau wengine kutuunga mkono ili kusaidia kufikisha ujumbe.
Lengo hili litatimia kwa kushirikiana na wadau katika kufanya operasheni
mbalimbali pamoja na kutoa elimu.” Alisema DCP Mpinga.
Mpinga
alitumia nafasi hiyo kuwaasa watanzania wote kote nchini kuepuka
kusafiri na kiwango kikubwa cha fedha badala yake watumie huduma ya
Airtel Money kutuma, kuweka na kutoa pesa.
Akizungumza kwa upande wake Balozi wa kampeni hizi za Usalama barabarani ambaye pia ni muhanga wa ajali za barabarani, Bw. Athumani
Hamisi alisema Kuelekea mwisho wa mwaka, matukio ya ajali za barabarani
yamekuwa yakiongezeka kutokana na ukiukwaji wa sheria, kanuni na
taratibu za usalama barabarani hivyo wananchi wanatakiwa kujitahidi
kutokiuka taratibu hizo.
“Ukiukwaji
wa sheria husababisha sana ajali za barabarani, wananchi wanapaswa
kuhakikisha wanafuata sheria za barabarani ili kuepusha ongezeko la
ajali hizo ambazo hutokea mara kwa mara haswa katika msimu huu wa
sikukuu.” Alisema Athmani.
No comments:
Post a Comment