




……………………………………………………………………………….
NA MAGRETH KINABO- MAELEZO
SERIKALI YASEMA TEHAMA KUFIKA HADI VIJIJINI
SERIKALI
imesema kwamba inatarajia kuboresha Teknolojia ya Habari na
Mawasiliano (TEHAMA) katika kila kijiji ili huduma zake ziweze kuwa
karibu na wananchi, hatua hiyo itasaidia kuwapunguzia gharama
wanazozitumia.
Aidha
Serikali imeeleza kwamba iteendelea kujenga uwezo wa kiufundi wa
kuweza kuzuia uvujaji wa siri, uhalifu na udhibiti wa sheria ndani
ya vyombo vyake ili taarifa za siri zisiweze kuvuja.
Kauli
hiyo imetolewa leo na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue
wakati alipotembelea ofisi ya Wakala ya Serikali Mtandao(e GA) jijini
Dares Salaam kwa ajili ya kuzungumza na menejimenti na wafanyakazi.
“Leo
nimetembelea ofisi hii. Ni eneo la kipaumbele kwa Serikali kwa
kuongeza matumizi ya TEHAMA kwa Serikali, tija, kasi ya utendaji kazi
na huduma za Serikali. Hivyo sehemu hii ni muhimu ya kuifanya Serikali
iwe karibu na wananchi. Tovuti hii iwe ni dirisha la mwananchi
kutatuliwa shida yake.,”alisema huku akitoa wito kwa wananchi wawe
tayari kuitumia.
Balozi
Sefue alisema tatizo la changamoto la TEHAMA kuhusu uvujaji wa
siri lipo dunia nzima hata Marekani wanakabiliana nalo ,hivyo
ufumbuzi wake si kuachana nalo bali kuzuia uvujaji huo na uhalifu kwa
kujenga uwezo wa udhibiti.
“Lazima
kuwe na udhibiti mfano wa kisheria tayari tunayo sheria tutaendelea
kuiboresha kulingana na changamaoto zitakazo kuja,” alisisitiza Balozi
Sefue.
Alisema
kupitia TEHAMA wananchi wataweza kupata matibabu au elimu na kulizia
huduma wanazotakiwa kuzipta mfano miradi ya visima vya maji imefikia
hatua zipi.
Aliongeza
kuwa hivi sasa wakala huo unaandaa mifumo ya kuwezesha Wizara, Idara na
taasisi mbalimbali za Serikali kufanya kazi kwa ushirikiano.
Akizungumzia
kuhusu ufikishaji wa huduma katika maeneo ya vijijini, Mtendaji Mkuu
wa (eGA) Dk. Jabiri Bakari alisema watatumia ubunifu ili kuhakikisha
huduma ya TEHAMA inatumika kwenye maeneo hayo mfano kwa kutumia sehemu
za mkononi za kawaida.
Wakala
hiyo ulianzishwa Julai mwaka 2012, ambapo taarifa mbalimbali za
Serikali kutoka Wizara, Idara , wakala na taasisi zake zitapatikana
kupitia mtandao wa wakala hiyo.
No comments:
Post a Comment