TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION

TANGAZO SHIWATA

Sunday, 15 September 2013

MABINGWA WA MKOA WA MOROGORO WA SAFARI POOL,ANATORY POOL CLUB,WATAMBA KUTWAA UBINGWA SAFARI POOL NATIONAL CHAMPIONSHIP 2013.



 Nahodha wa klabu ya Anatori, Athumani Selemani(kulia) na Harid Mohamed wakishindana kulagi wakati wa mazoezi wakijiandaa na fainali za mashindano ya Pool Taifa yanayotarajiwa kufanyika Mkoani Morogoro Septemba 19-22,2013 katika ukumbi wa Tanzanite.
Nahodha wa klabu ya  Pool ya Anatory,Athumani Selemani akilagi
 Harid Mohamed akicheza

ANATORY WATAMBA KUTWAA UBINGWA WA SAFARI POOL TAIFA 2013.
MKURUGENZI wa Klabu ya mchezo wa Pool ya Anatory, Anatory Makasi ametamba kutwaa Ubingwa wa fainali za mashindano ya Pool Taifa kwa mwaka huu  wa 2013.
Anatory ameyasema hayo leo jioni alipotembelewa na mtandao huu kujua maandalizi yake kama mwenyeji wa fainali za mashindano ya Safai Pool Taifa 2013, ambayo kwa mwaka huu yanatarajiwa kufanyika mkoani Morogoro.
Anatory amesema anakilasababu za kutwaa ubingwa huo kwani amejiaandaa vizuri,alikuwa na kambi katika mikoa tofauti ikiwemo Dodoma na Taanga na sasa vijana wako kambini wakiendelea na mazoezi makali kuikabili mikoa 16ikiwakilishwa na vilabu 16 inayotarajiwa kuwasili kuanzia Septemba 15 na 16 mwezi huu.
Alisema Anatory vijana wako vizuri hawana shida kabisa wanachosubiri ni kukamilisha adhima yao ya kutwaa Kikombe na na fedha taslimu shilingi 5,000 000/=  kama mabingwa wa “Safari Pool National Championship 3013”.
Kosi kuwajuza kuwa Morogoro pako swari,amani tele,usalama upo wa kutosha,hali ya hewa nzuri kabisa hakuna joto hivyo wachezaji wote pamoja, viongozi na mashabiki wanakaribishwa Morogoro.
Nae Nahodha wa Klabu ya Anatory,Athuman Selemani alikitaja kikosi chake anachokiongoza kuwa ni Harid Mohamed,Six Timbulo,Alfan Ngassa,Juma Kassim,Juma Ally,Charles Philipo na Mussa Mkwanga.Ambapo viongozi ni Mwenyekiti Jackson Philipo,Katibu Mohamed Makanyaga na Mkurugenzi Anatory Makasi.

No comments:

Post a Comment