TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION

TANGAZO SHIWATA

Wednesday, 25 September 2013

KIKUNDI CHA CASH MONEY WACHANGIA DAMU HOSPITALI YA TEMEKE


UVAAJI wa nepi za kutupa (Pampers), umechangia kwa kiasi kikubwa
ongezeko la ugonjwa wa U.T.I kwa watoto.
Akizungumza na waandishi wa habari, Hospitali ya Wilaya ya Temeke, Dar
es Salaam jana,  muuguzi mkuu wa wodi ya watoto katika hospitali hiyo,
Nuswe Ambokile alisema wamekuwa wakipokea idadi kubwa ya watoto wenye
ugonjwa huo kila siku.
"Wodi yetu ina uwezo wa kulaza watoto 34, lakini tumekuwa tukilaza
hadi 100 na zaidi, wakiwemo wa U.T.I, hali inayofanya wengine walale
watatu katika kitanda kimoja,"aliongeza.
Alisema magonjwa mengine yanayowasumbua watoto ni pamoja na Nimonia
(vichomi), kuharisha, majeraha ya moto na ajali na ugonjwa wa Malaria.
Aliwataka wahisani mbalimbali kujitokeza kusaidia wodi hiyo, ambayo
ina mahitaji makubwa ya upanuzi wa jengo, vitanda, vyandarua, vifaa
vya kazi na masihine za Oxygen.
"Hata wauguzi, maana wapo wachache mno, na wakiondoka zamu, tunabaki
wawili au watatu ambao hatumudu kuhudumia watoto zaidi ya 100, kwani
kwa wastani tunaweza kupokea hadi watoto 20 kwa siku,"alisema Nuswe.
Naye Meneja wa maabara katika hospitali hiyo, Grace Maliva, alisema
wanahitaji watu mbalimbali kujitokeza na kujitolea damu, kwani kuna
vifo vingi vya watoto na wanawake wajawazito vinavyotokea kutokana na
kukosa damu.
"Tatizo la damu ni kubwa, na tumekuwa na vikundi viwili tu ambavyo
hutuchangia damu, kikiwemo Cash Money na Shia, hivyo tunahitaji
kampuni na taasisi mbalimbali zijitokeze na kuchangia damu,"
aliongeza.
Katika hatua nyingine, kundi la wajasiriamali la Cash Money, jana
lilitoa vitu mbalimbali kwa wodi ya watoto vikiwemo sabuni, vyandarua,
vitu vya kuchezea watoto, ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa kundi hilo

No comments:

Post a Comment