Kampuni
ya Glitz Entertainment imeandaa Toto Party kwa ajili ya watoto wa jiji
la Dar es Salaam na vitongoji vyake linayotarajiwa kufanyika katika Art
Gallery iliyopo Mbezi Beach siku ya Iddi Mosi.
Akizungumza na waandishi
wa habari jijini Dar es Salaam muandaaji wa tamasha hilo, Deniss Ssebo
alisema kuwa hii ni mara ya nne kuandaa TOTO PARTY kwa ajili ya watoto,
na wanatarajia kuanza kulipeleka na mikoani.
Katika
Tamasha hilo, watoto watapata nafasi ya kushiriki katika michezo
mbalimbali kama soka,kuogelea, kusaka hazina (Treasure hunt) na
kujipaka rangi usoni (Face painting) na mengine mengi.
Aidha watoto hao pia wataweza kukutana na wenzao wanaoishi katika mazingira magumu.
Aidha watoto hao pia wataweza kukutana na wenzao wanaoishi katika mazingira magumu.
Mbali
na watoto kucheza na kufurahi michezo mbalimbali pia wazazi wao
watachuana katika mchezo wa kuvuta kamba ambapo washindi katika michezo
hiyo watazawadiwa zawadi mbalimbali na viingilio ni Sh 3,000 kwa watoto
na wakubwa Sh 7,000.
No comments:
Post a Comment