TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION

TANGAZO SHIWATA

Thursday, 29 August 2013

MTANZANIA ASHINDA TUZO YA “BEST TOURISM PROMOTER OF THE YEAR” KWA KUITANGAZA VIZURI HIFADHI YA NGORONGORO



Mmiliki na mwendeshaji wa mashindano ya urembo ya Miss East Africa ambae ni mtanzania, ndg. Rena Callist ameshinda tuzo ya heshima ya MBE Improver Awards huko ulaya na kuwa raia aliyeitanza Nchi yake kimataifa kuliko wote barani Africa kwa mwaka 2012 hadi 2013.
Rena Callist Amejishindia tuzo hiyo jumamosi iliyopita baada ya kupigiwa kura na watu mbalimbali Duniani  baada ya kuitangaza Nchi ya Tanzania kwa kuonyesha vivutio vyake vya utalii kupitia katika mashindano yake ya Miss East Africa yaliyofanyika mwaka jana na kurushwa kwa television “LIVE” Dunia nzima ambapo vivutio vya Tanzania vilionyeshwa hususan Hifadhi ya Ngorongoro ambayo ilitangazwa kwa kiasi kikubwa kupitia mashindano hayo.
 
Tuzo hiyo ya heshima iliyotolewa katika ukumbi wa  Bijlmer Park Theatre, jijini Amsterdam Uholanzi wiki iliyopita, na kuhudhuriwa na watu mbalimbali maarufu kutoka ndani na Nje ya Ulaya na kurushwa hewani na Television ya Dutch TV

“MBE Improver Awards is to acknowledge, celebrate and confer excellence on individuals who devoted their all in promoting human welfare and advancing reforms in their specific fields, not forgetting our cultural heritage, Tourism and what we as humans stand for”  alisema Sola Opesan Brown ambae mmiliki wa gazeti la Black European Gossip la uholanzi na ambae ni muandaaji wa tuzo hizo na kusema kwamba Rena Callist kutoka Tanzania ameshinda Tuzo hiyo baada ya kupigiwa kura nyingi na watu mbalimbali wanaofuatilia kazi zake za kuitangaza Tanzania.

Ola Opesan alitolea mfano ukurasa wa facebook wa “Tourism Tanzania" wa Rena Callist na kusema ukitizama picha zake katika page hiyo lazima utashawishika kuitembelea Tanzania kwa sababu picha zake zinavutia sana na inaonyesha jinsi anavyofanya bidii kubwa ya kuitangaza Tanzania kimataifa.

Katika tuzo hizo Rena aliwashinda watu wengine maarufu kutoka Africa waliokuwa wakipigiwa kura ili kuiwania tuzo hiyo wakiwemo Ndg. Wale Ojo Lanre wa Tribune Tourism magazine wa Uingereza na Ngd. Oladimeji Adisa ambae ni mkurugenzi wa "Come to Nigeria”

Tuzo hiyo ya Rena Callist ilikabidhiwa kwa ubalozi wa Tanzania Nchini Uholanzi na anatarajiwa kukabidhiwa Rasmi hapa Nchini hivi karibuni.

Nawashukuru wote walionipigia kura, Tuzo hiyo ni heshima kwangu na kwa Nchi yangu.....nawaomba watanzania wote tuungane kuitangaza Nchi yetu, na pia sisi wenyewe tujenge utamaduni wa kutembelea vivutio vyetu vya utalii kwa mfano hifadhi ya Ngorongoro ni sehemu ambayo inatupasa wote kuitembelea kwa sababu ni chimbuko la asili ya uhai wa binadamu duniani....” Rena Callist

Wengine walioshinda Tuzo mbalimbali za MBE Improver awards 2013 ni pamoja na MBE ROYAL FATHER AWARD iliyokwenda kwa

His Royal Highness The King, Oba Adeyemi Adediran, The Omiran of Esa Oke Kingdom, Osun State of Nigeria.

No comments:

Post a Comment