TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION

TANGAZO SHIWATA

Saturday, 3 August 2013

Makamu wa Rais Dk Bilal ahudhuria kuapishwa Rais Mpya wa Iran




 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Viongozi mbalimbali wa Serikali ya Jamhuri ya Kiislam ya IRAN alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Teheran leo Ogast 03-2013 kwa ajili ya kuhudhuria kuapishwa kwa Rais Mpya wa Nchi hiyo Bw. Hassan Rouhan  Al-Quds  anayetarajiwa kuapishwa kesho baada ya kushinda kwenye uchaguzi Mkuu uliomalizika hivi karibuni.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Mshauri Maalum wa Waziri wa Mambo ya nje wa Serikali ya Jamhuri ya Kiislam ya IRAN bw. Mohammad Valulleh kwenye chumba maalum cha mapumziko VIP katika  uwanja wa ndege wa kimataifa wa Teheran leo Ogast 03-2013 alipowasili Nchini Irani kwa ajili ya kuhudhuria kuapishwa kwa Rais Mpya wa Nchi hiyo Bw. Hassan Rouhan Al-Quds  anaetarajiwa kuapishwa kesho baaada ya kushinda  kwenye Uchaguzi Mkuu uliomalizika hivi karibuni.

No comments:

Post a Comment