TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION
TANGAZO SHIWATA
Monday, 5 August 2013
Bandari Sacco ya Kenya yatembelea Tazara Saccos
Na Mwandishi Wenu
VIONGOZI wa Chama cha Kuweka na Kukopa cha Bandari Sacco Ltd cha Kenya kimevisifu vyama hivyo nchini kwa kuwajali wanachama wao kukopa fedha nyingi naurejesha kwa riba kidogo.
Mwenyekiti wa Bandari Sacco Ltd ya Kenya, Bw. Gerald Ojung'a ya Kenya alisema jana Dar es Salaam kuwa mfumo wa utoaji mikopo kwa wanachama kwa kuwatoza riba kidogo inawapa nafasi ya kuvipenda vyama vyao badala ya kukimbilia benki ambako kuna riba kubwa.
Akizungumza na wanachama cha Tazara Karakana Saccos Bw. Ojung'a alisema ziara hiyo ambayo imejumuisha viongozi 72 kutoka Bandari ya Mombasa, Kisumo na bandari kavu ya Nairobi ni mafunzo yatakayoboresha utendaji wao.
Mwenyekiti wa Tazara Karakana Saccos, Bw. Bundala Kabulwa alisema ushirika huo wenye mtaji wa sh. milioni 90,inao wanachama 60 wanapata huduma ya mikopo ya dharura,mikopo ya maendeleo na wanaarajia kuanzisha Benki ya Saccos.
Bw. Bundala alisema Tazara Karakana Saccos pia imefungua duka na kutoa huduma za Tigo Pesa, M-Pesa na kujenga nyumba ya ushirika huo ambao litamilikiwa na ushirika huo.
Katika ziara hiyo ujumbe wa wanachama wa Bandari Sacco Ltd ya Kenya pia walitembelea Magereza Saccos na Bandari Saccos ambako nako waliona mafanikio ya ushirika huo.
Mwenyekiti wa Magereza Saccos, Bw. Joel Bukuku alisema wanachama wao wanaweza kukopa mara tatu ya akiba na kurejesha kwa riba kidogo.
Alisema Magereza Saccos inaundwa na askari wa Jeshi la Magereza na waliosaafu inayo mtaji wa sh. Bil. 8.7 na wanachama 11,860 nchi nzima.
mwisho
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment