TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION

TANGAZO SHIWATA

Wednesday 17 July 2013

Zuku yawazawadia washindi wake Tamasha la Ziff

Na Mwandishi Wetu
 

KAMPUNI ya Zuku imekabidhi zawadi ya fedha kwa washindi watano walioibuka kidedea katika tuzo za Zuku Bongo Swahili Movie awards katika tamasha la ZIFF.
 

Mwenyekiti wa Wananchi Group, Ali Mufuruki akikabidhi fedha hizo jana alisema tuzo hizo ambazo zilikuwa  maalumu kwa ajili ya filamu za Kiswahili zilihusisha vipengele vya Muigizaji bora Kike ambapo muigizaji Elizabeth Michael aliyeigiza katika filamu ya Woman of Principles alishinda.

Aliema msanii Bond Bin Suleiman aliibuka na tuzo mbili ikiwa ni pamoja na tuzo ya Muigizaji bora wa kiume katika filamu ya Lovers’ Island na tuzo ya muongozaji bora wa filamu katika filamu hiyo hiyo ya Lovers’Island.

Pia tuzo ya filamu bora ilinyakuliwa na Javed Jaffery ambaye ndiye mtengenezaji wa filamu ya Lover’s Island. Filamu ya Shoeshine ya Amil Shivji ilitwaa tuzo ya People’s choice .

Alisema filamu  bora iliondoka na kitita cha sh. milioni moja na kwa vipengele vingine kila mshindi aliondoka na kitita cha shilingi laki tano.  

 "Tunafurahi kwamba katika mwaka wetu wa pili wa udhamini ZIFF tumeweza kujumuisha tuzo maalumu za Zuku kwenye tamasha la ZIFF. Tuzo hizi ambazo zilikuwa maalumu kwa ajili ya filamu za Kiswahili, hazitoi mwanya tu kwa washindi kupata zawadi bali pia kuboresha kazi zao na kuzifanya ziwe na viwango vya kimataifa” alisema Mufuruki.

 Naye Meneja wa Zuku Tanzania Fadhili Mwasyeba alisema kwamba Zuku inafanya jitahada za kuzawadia  filamu za Kiswahili na pia kutambua jitihada za wasimuliaji wazuri wa hadithi wazawa kupitia sanaa ya filamu wakiamini kuwa tuzo hizo zitachangia ukuaji wa sekta ya filamu.

 Vigezo vilivyo tumika katika kupata filamu bora vilihusisha  ubora wa kazi,simulizi na mchezaji, uigizaji na uelekezaji wa filamu, Majaji walitumia miongozo na maelekezo ya ZIFF katika kumtafuta mshindi.

 Katika kutafuta Muigizaji bora wa kike na muigizaji bora wa kiume, vigezo vilivyotumiwa ni pamoja na uelewa wa script, kujituma kujenga hisia,kutoa utendaji ambayo ni mzuri kwa ufanisi wa uzalishaji wa jumla wa utendaji.

mwisho






No comments:

Post a Comment