Mwakilishi
wa Afisa Utamaduni Mkoa wa Shinyanga,Seif Hamadi(kushoto)na Mwenyekiti wa Chama
cha Pool Shinyanga, Jastin Shine (wapili kushoto) wakimkabidhi nahodha wa Klabu
ya King Palace, Kulwa Peter, fedha taslimu shilingi 700,000 mara bada ya
kuibuka mabingwa kwenye fainali za mashindano ya Safari Pool Taifa Ngazi ya
Mkoa yaliyofanyika katika Klabu ya Garden Mkoani Shinyanga
Machezaji wa Klabu ya King Palace wakishangilia na kitita cha shilingi 700,000 mara baada ya kuibuka mabingwa kwenye fainali za mashindano ya Safari Pool Taifa Ngazi ya Mkoa yaliyofanyika katika Klabu ya Garden Mkoani Shinyanga
FAINALI za
mashindano ya mchezo wa Pool Taifa ngazi ya Mkoa yanayodhaminiwa na Kampuni ya
Bia nchini(TBL) kupitia Bia ya Safari Lager yamemalizika vyema kwa kupata
vilabu vitakavyowakilisha mikoa katika mikoa mine ambayo ni Shinyanga,Kilimanjaro,Kagera
naTabora.
Mkoa wa
Shinyanga,King Palece klabu wameibuka
mabingwa 2013, baada ya kumfunga klabu ya Emerates 13-8.Kwa ubingwa huo
walizawadiwa fedha taslimu shilingi 700,000/= na tiketi ya kuwakilisha Mkoa wa
Shinyanga kwenye fainali za kitaifa zinazotarajiwa kufanyika Mkoani Morogoro
mwezi ujao. Emirates walikamata nafasi ya pili na kuzawadiwa fedha taslimu
shilingi 350,000/=,Nafasi ya tatu ni Klabu Veteran ambao walizawadiwa shilingi
200,000/=.
Upande wa
wachezaji mmoja mmoja(Singles) wanaume,Paul Silas alitwaa ubingwa kwa kumfunga
Siga Agustino 3-0,hivyo kuzawadiwa fedha taslimu shilingi 350,000/= pamoja na
tiketi ya kuwakilisha Mkoa kwenye fainali za kitaifa Mkoani Morogoro ambapo
Siga alikamata nafasi ya pili na kuzawadiwa fedha taslimu shilingi
200,000/=.Upande wa wakinadada Sada Tula alitwaa ubingwa na kuzawadiwa fedha
taslimu shilingi 250,000/=
Mkoa wa
Kilimanjaro, Klabu ya
Mbosho imefanikiwa kutetea ubingwa wa
Mashindano hayo kwa kuifunga Goodhope 16-5 na hivyo kujinyakulia zawadi ya
fedha taslimu shilingi 700,000/= na Medali ya Dhahabu pamoja na tiketi ya kuwakilisha Mkoa kwenye fainali za kitaifa pale Morogoro,na nafasi ya poli ilichukuliwa na Goodhope ambao
walizawadiwa shilingi 350,000/= na
medali ya Fedha.Nafasi ya tatu ilichukuliwa na Highbury na kuzawadiwa fedha
taslimu shilingi 200,000.
Katika mchezo wa mchezaji mmoja mmoja (Singles) wanaume mchezaji, Peter George alifanikiwa kutwaa ubingwa na kuzawadiwa fedha taslimu shilingi 350,000 na tiketi ya kuwakilisha mkoa kwenye fainali za kitaifa baada ya kufunga Spider Elisha 2-1ambaye alikamata nafasi ya pili na kuzawadiwa shilingi 200,000.
Upande wa wanawake mchezaji, Mwayamu Mwinyi alitwaa ubingwa na kuzawadiwa shilingi 250,000 na tiketi ya kuwakilisha mkoa kwenye fainali za kitaifa Mkoani Morogoro baada ya kumfunga, Maya Saburi 2-1 ambapo yeye alishika nafasi ya pili na kuzawadiwa shilingi 150,000.
Mkoa wa Kagera,Klabu ya Bilele ilitwaa ubingwa na kuzawadiwa fedha taslimu shilingi 700,000 na tiketi ya kuwakilisha Mkoa kwenyefainali za kitaifa baada ya kuifunga Klabu ya Bukoba ambayo ilishika nafasi ya pili na kuzawadiwa fedha taslimu shilingi 350,000.Nafasi ya tatu ilichukuliwa na Klabu ya Q Bar ambao walijinyakulia fedha taslimu shilingi 200,000.
Upande wa
mchezaji mmoja mmoja wanaume,Gozbat Kapama alitwaa ubingwa na kuzawadiwa
shilingi 350,000 na tiketi ya kuwakilisha Mkoa kwenye fainali za kitaifa na
Upande wa wanawake mmoja mmoja Patricea Parick alitwaa ubingwa na kuzawadiwa
250,000 na tiketi ya kuwakilisha mkoa kwenye fainali za kitaifa.
Mkoa wa
Tabora,Kalbu ya Loriondo wameliibuka mabingwa na kuzawadiwa shilingi 700,000
pamoja na tiketi ya kuwakilisha mkoa kwenye fainali za kitaifa wakati nafasi ya
pili ilichukiwa na Klabu ya Tiptop ambao walijinyakulia frdha taslimu shilling
350,000.
Upande wa
mchezaji mmoja mmoja wanaume,Ernest John alitwaa ubingwa na kuzawadiwa shilingi
350,000 na tiketi ya kuwakilisha mkoa kwenye fainali za kitaifa wakati upande
wa kinadada,Happness Magani alitwaa ubingwa na kuzawadiwa shilingi 250,000 na
tiketi ya kuwakilisha mkoa kwenye fainali za kitaifa Mkoani Morogoro.
No comments:
Post a Comment