Na Peter Mwenda
MBUNGE
wa Temeke, Bw. Abbas Mtemvu amesema benki za kigeni hazijawahi
kuwasaidia wajasiriamali wa Tanzania kutokana na riba kubwa zinazotozwa
baada ya kutolewa mikopo.
Akizungumza
katika uzinduzi wa kikundi cha VICOBA cha Safina cha Keko juzi, Bw.
Mtemvu alisema riba zinazotozwa na mabenki ya nje inawanufaisha wenyewe
lakini wajasilimali wa Tanzania ambao wanahaha kutafuta mitaji
wanashindwa kupata mikopo ya riba ndogo.
"Mabenki
yote hayana msaada, yamekuja kuchuma tu na siyo kusaidia watanzania,
serikali inatuambie tuanzishe VICOBA lakini mitaji tutapata wapi?alisema
Bw. Mtemvu.
Alisema
mikopo iliyotolewa na Rais Jakaya Kikwete maarufu kama mabesa ya JK
yamekqwenda kwa vigogo wachache na kuwaacha wananchi wa kawaida wenye
nia ya kujikwamua kimaisha kwa kuanzisha miradi bila kujua zilikwenda.
Bw.
Mtenmvu alisema benki ambazo zilianzishwa kwa ajili ya wananchi nazo
zimebadilisha mwelekeo badala yake uzinawakopesha matajiri hivyo
kuwaacha wananchi wa kawaida wakikwama kutokana na kukosa mitaji ya
biashara.
Mbunge
huyo mbaye pia ni Mwenyekiti wa wabunge wa mkoa wa Dar es Salaam
alisema katika VICOBA nako kumezuika tabia ya baadhi ya viongozi kukaa
na fedha za wanachama wao bila kupeleka benki.
Alisema atatumia nafasi hiyo kuwachukulia hatua viongozi wa VICOBA ambao hawajafungua akanti benki kwa ajili ya kuweka fedha za
wanachama.
Mwenyekiti
wa kikundi cha Vicoba cha Safina,Bw. David Nyambe alisema mikakati yao
ya awali na kununua gari la wagonjwa na kuanzisha kikundi cha kuzoa taka
katika eneo la Keko.
Alisema
kikundi hicho kimenunua hekari 50 wilayani Rufiji na kina mtaji wa sh.
mil. 29 kwa ajili ya kukopesha wanakikundi ambao hautoshi
kukopa mara tatu zaidi.
Naye
mratibu wa asasi ya UYACODE, Bw. Aldo Mfinde alisema ili kupunguza
umaskini nchini ni pale ambapo wananchi wataamua kujiunga kuanzisha
vikundi vya VICOBA
mwisho
No comments:
Post a Comment