Na Elizabeth John
MKALI wa muziki wa kizazi kipya
nchini, Peter Msechu, ameachia kibao chake kipya kinachokwenda kwa jina la ‘Kibudu’
ambacho kimeanza kufanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio.
Mbali na kutamba na kibao hicho,
mkali huyo alishawahi kutamba na kibao chake cha ‘Relax’, ‘Kumbe’ ambavyo vilifanya
vizuri zaidi mbali na kuwa na vibao vingi ambavyo vilimtambulisha katika tasnia
ya muziki huo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Msechu alisema kazi hiyo imekamilika na tayari
imeanza kufanya vizuri katik avituo mbalimbali vya redio.
Alisema kibao hicho kakitengeneza
katika studio ya Ufundi Production chini ya mtayarishaji wake mahiri, Fundi
Samuel.
“Naomba mashabiki wangu wakipokee
vizuri kibao hicho ambacho natarajia kukifanyia video yake Nairobi, Kenya,”
alisema.
No comments:
Post a Comment