TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION

TANGAZO SHIWATA

Wednesday, 31 July 2013

BENKI YA NBC YAFUTURISHA WATEJA WAKE WA ZANZIBAR

Rais wa Zanzibar  na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dr Ali Mohamed Shein (wa tatu kushoto), akiwa na Makamu Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd (wa pili kushoto), Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya NBC, Dk Mussa Assad (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji NBC, Mizinga Melu katika hafla ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo kwa wateja wake mjini Zanzibar jana.

Rais wa Zanzibar  na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dr Ali Mohamed Shein (kulia), akichukua futari katika hafla iliyoandaliwa na Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) mjini Zanzibar jana.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd (kulia) akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji  wa Benki ya NBC, Bi. Mizinga Melu katika hafla ya futari  iliyoandaliwa na Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa wateja wake mjini Zanzibar jana. Kushoto ni Meneja Mkuu Kitengo cha Uhusiano cha benki hiyo, William Kallaghe.

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali  wa Zanzibar, Zahra Ali Hamadi (kulia), Katibu Mkuu katika wizara hiyo, Mwanaidi Saleh  Abdallah (katikati) na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Mizinga Melu (kushoto) wakichukua mlo wa futari iliyondaliwa na benki hiyo mjini Zanzibar jana.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd (kulia) akilakiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya NBC, Dk Mussa Assad katika hafla ya futari  iliyoandaliwa na NBC Kwa wateja wake mjini Zanzibar jana. Katikati ni Meneja Mkuu Kitengo cha Uhusiano cha benki hiyo, William Kallaghe.

Mjumbe wa Bodi ya Benki ya NBC, Dk Kassim Hussein (kulia) akiagana na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Abdallah Mwinyi Khamis baada ya hafla ya futari waliyoiandaa kwa wateja wao mjini Zanzibar jana. Nyuma ya Dk Kassim ni Mkurugenzi Mtendaji wa NBC Tanzania, Mizinga Melu.

Baadhi ya waalikwa katika hafla ya futari iliyoandaliwa na Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) Kisiwani Zanzibar jana.

MANENO MBEGU NA QUEEN SENDIGA WAMEREMETA

 Bwana Harusi Maneno Mbegu akivishwa pete na mwandani wake, Queen Sendiga walipokuwa wanafunga ndoa hivi karibuni katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam.
                     Maneno Mbegu akiapa mbele Ofisa Tawala  Wilaya ya Kinondoni
                                    Queen akila kiapo
                                Mbegu akitia saini
 Queen akitia saini
Wakitoka baada ya kufunga pingu za maisha
Du! hivi kweli tumeoana?
                                                Maharusi wakiwa na sura za bashasha
Huyu ndiye Mbegu
Baba akimpongeza binti yake kwa kuolewa
Mbegu na mkewe Queen akiw na katika picha ya pamoja na wakwe zake.
Maharusi wakiwa katika picha ya pamoja na ndugu zao pamoja na marafiki

Queen anavyomeremeta
Queen akiwa na mamake mzazi katikati na mdogo wake
Queen akiwa na watoto wapambe
No comments:

No comments:

Post a Comment