TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION

TANGAZO SHIWATA

Tuesday, 25 June 2013

GRAND MALT YAKABIDHI VIFAA VYA MICHEZO KWA TIMU ZA BARAZA LA WAWAKILISHI ZANZIBAR



Makamu wa pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Balozi Seif Ally Iddy, akipokea vifaa mbalimbali vya michezo kwa timu za Baraza la Wawakilishi za mpira wa miguu na pete kutoka kwa Meneja masoko wa kinywaji cha Grandmalt  Fimbo Mohamed Butallah, wakati wa makabidhiano yaliyofanyika kwenye ukumbi la baraza la wawakilishi Zanzibar, kushoto kwake ni mwenyekiti wa timu ya Baraza la wawakilishi mheshimiwa Hamza Hassan Juma. Picha kwa Hisani ya Intellectuals Communications Limited.
**********************************************
WAKATI HUO HUO:- MAANDALIZI YA TAMASHA LA GRAND MALT YASHIKA KASI ZNZ
Na Mwandishi Wetu
HUKU zikiwa zimebaki siku chache kabla ya kufanyika kwa Tamasha la Wazi la Filamu Tanzania, maarufu kama ‘Grand Malt Tanzania Open Film Festival’ ambalo litafanyika katika Viwanja vya Sahara jijini Mwanza, maandalizi yake yamezidi kupamba moto.

Mratibu wa Tamasha hilo aliye pia Mkurugenzi wa Sophia Records, Musa Kissoky, alisema kwa sasa kila kitu kimekamilika na kinachosubiriwa ni kuanza kwa tamasha hilo Jumatatu ijayo.
Kissoky alisema, tamasha hilo ambalo litakuwa la bure kwa watu wote na kushirikisha mastaa wa filamu hapa nchini, litakuwa la aina yake kwani vitu vitakavyofanyika vitakuwa si vya kawaida.

“Kwa sasa maandalizi yamekamilika kwa asilimia 90, yaani tunaleta kitu tofauti ambacho watu watashangaa, ndio maana mpaka sasa wengi wanapigwa na bumbuwazi kuhusu kile tutakachofanya siku hiyo,” alisema.
Naye Meneja wa kinywaji cha Grand Malt walio wadhamini wakuu wa tamasha hilo, Consolata Adam, alisema wameamua kufanya kweli zaidi kwani wanataka kuona Watanzania wanapata kitu chenye uhakika.
“Tumejipanga katika hili na wala hatutanii kwani tunataka kuwawezesha wakazi wa Mwanza na maeneo ya jirani kuhudhuria tamasha hili kwa wingi . Tunawakaribisha watu wote wenye mapenzi na filamu zetu za Tanzania kufika na kushuhudia tamasha hili ambalo mwaka huu limeboreshwa zaidi,” alisema Consolata.
Naye Meneja Habari na Mawasiliano wa TBL, Edith Mushi, alisema, kutokana na ubora wa kinywaji cha Grand Malt hata tamasha hilo litakuwa la aina yake na litakaloiteka mikoa yote ya Kanda ya Ziwa.
“Tumeona jinsi wananchi wanavyozipenda filamu za Tanzania, maarufu kama ‘Bongo Movies’ na jinsi walivyo na kiu ya kuwaona wasanii wa filamu ana kwa ana, sasa  kazi kwao kuwashuhudia na kuona tamasha bora zaidi,” alisema.
Tamasha la Filamu la Grand Malt linatarajiwa kuanza Julai 1-7, mwaka huu huku kukiwa na filamu mbalimbali zitakazooneshwa katika kipindi hicho. Filamu zote hizo ni kutoka Tanzania.
Wasanii wakali wa Bongo Muvi wakiwemo Aunty Ezekiel, Vicent Kigosi ‘Ray’, Jacqueline Wolper, Irene Uwoya, Jacob Steven ‘JB’, Mahsein Awadh ‘Dk Cheni’na  Issa Mussa ‘Cloud’ ni baadhi ya wasanii walioahidi kufanya kweli pia katika tamasha hilo.
Tamasha hilo la filamu limedhaminiwa na kinywaji cha Grand Malt kisicho na kilevi ambacho kinazalishwa na kusambazwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).

No comments:

Post a Comment