Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akipokea mic kutoka kwa
msanii wa muziki wa kizazi kipya, Mataluma baada ya kumtaka aanza kuimba
kabla ya msanii huyo kuanza kutoa burudani wakati wa uzinduzi wa huduma
mpya ya Wakala wa benki hiyo.
Wacheza shoo wakionesha manjonjo yao.
DAR ES SALAAM, Tanzania
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akiimba kibao cha Mataluma kinachokwenda kwa jila la ‘Tunasonga Mbele’.
Mataluma akiimba kwa hisia wimbo wa CRDB 'Tunasonga Mbele'Wacheza shoo wakionesha manjonjo yao.
DAR ES SALAAM, Tanzania
MSANII wa Bongo fleva kutoka Nyumba ya Vipaji Tanzania
(THT), Mataluma na wacheza shoo wa kundi hilo, walishindwa kuamini baada ya Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB, Dk. Charles
Kimei kueleza nia ya kununua kibao cha ‘Tunasonga Mbele’.
Kibao hicho kilichotungwa na Mataluma kwa ajili kupamba
uzinduzi wa mfumo mpya wa kuhudumia wateja wa CRDB wa FahariHuduma, kilimvutia
mno Dk. Kimei na kuagiza idara husika kukaa na msanii huyo kufanya mazungumzo
ya kukinunua.
“Nimevutiwa mno na ubunifu uliofanywa na mtunzi katika kibao
hiki na ningependa kuona CRDB inakimiliki na kukitumia katika matangazo yetu
tofauti, hivyo naiagiza idara husika kukaa na Mataluma na kumlipa, ili asije
kukitumia mahali pengine,” alisema Dk. Kimei.
Uamuzi huo ulipokelewa kwa shangwe kutoka kwa waalikwa wa
uzinduzi huo, uliofanyika hoteli ya Kempinski, huku wacheza shoo wa THT na
Mataluma wakipagawa kutokana na agizo hilo
ambalo hawakulitegemea.
Akizungumza baada ya agizo hilo la Dk. Kimei, Mataluma alikiri
kufurahishwa kuona utunzi huo umewavutia wengi ukumbini kiasi cha mkurugenzi
huyo kukihitaji moja kwa moja, na kwamba anaamini mazungumzo baina ya pande
mbili yatafikia muafaka.
“Nina kila sababu ya
kufurahi, kutokana na siku hii kuwa ya aina yake kwangu kama
msanii. Namshukuru Dk. Kimei kwa kuvutiwa na kuthamini kilichofanywa katika
kibao hiki maalumu kwa ajili ya hafla hii ya uzinduzi wa FahariHuduma ya CRDB,”
alisema Mataluma.
No comments:
Post a Comment