TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION

TANGAZO SHIWATA

Tuesday 12 February 2013

Mtaa wa Ukombozi wazaliwa Kivule, Ilala

Na Peter Mwenda

WAKAZI 3,000 wa eneo la Ukombozi Kata ya Kivule wameiomba Serikali kuwashirikisha katika kuleta maendeleo ya eneo hilo baada ya kesi iliyokuwa imewatenganisha kati yao na Umoja wa Vijana wa Kikristo Tanzania (UVIKIUTA) kumalizika.

Akizungumza kwenye mkutano wa wananchi uliowachagua viongozi wa eneo hilo, Mwenyekiti wa kamati hiyo Bw. John Anania alisema wameteseka kwa muda mrefu wakikosa ushirikiano lakini Mahakama imetoa hukumu kuwa wao ni wakazi halali.

"Kutoka mwaka 2008 tumekuwa tukisumbuka kuambiwa hili ni eneo la UVIKIUTA na kuvunja nyumba zetu tumehangaika mahakamani na sasa tumehalalishwa kuwa sisi ni wakazi halali" alisema Bw. Anania.

Katika mkutano huo uliosimamiwa na Mwenyekiti wa Mtaa wa Kivule, Bw. Joseph Gassaya wananchi hao walisema imefika wakati Serikali iungane na wananchi wake baada ya kuwatenga kwa muda mrefu.

Katibu wa Kamati hiyo, Bw. Chacha Marwa "kibendera" alisema wakazi wa eneo hilo wameteseka kwa muda mrefu  wakitakiwa wahame na wengine kuvunjiwa nyumba zao wakidaiwa ni wavamizi lakini ukweli umebainika kuwa wao ni wanaishi kihalali.

Viongozi waliochaguliwa ni John Anania (Mwenyekiti), Kibendera (Katibu) na Wajumbe wanne ambao ni Bw. Ramadhani Madisa,Mchungaji Robert Msae,Bi. Asteria Chacha na Bi. Anastazia Chacha.

Awali akiwatoa hofu wakazi hao Mwenyekiti wa mtaa wa Kivule, Bw. Gassaya alisema serikali haijawatupa wananchi hao na kuwataka wawe wavumilivu wakati ufumbuzi wa malalamiko yao unafanyiwa kazi.

mwisho 






 

No comments:

Post a Comment