TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION

TANGAZO SHIWATA

Saturday, 12 January 2013

MWANARIADHA WA KENYA AFANYIWA KITU MBAYA BRAZIL



SAO PAULO, Brazil MWANARIADHA Edwin Rotich wa Kenya juzi alifanyiwa kitu mbaya baada ya kuvamiwa na mtu anayedaiwa kuwa na matatizo ya akili wakati alipokuwa akishiriki katika mbio za kimataifa za kilometa 10 nchini Brazil.

Rotich alikumbwa na mkasa huo wakati alipokuwa akiongoza mbio hizo na kubakiza kilometa chache kabla ya kumaliza.

Mtu huyo, aliyetajwa kwa jina la Wallace de Sousa (33) alimvamia Rotich kwa lengo la kumwangusha, lakini mwanariadha huyo alipambana naye kiume na kufanikiwa kujinasua.

Wakati Wallace alipokuwa akitaka kumvamia Rotich kwa mara ya pili, polisi watatu waliokuwa kwenye pikipiki walifanikiwa kumuokoa na kumtia mbaroni mtu huyo.

Kwa mujibu wa polisi wa Brazil, tukio hilo lilitokea katika mtaa wa Cuiaba, ambapo Wallace alikuwa miongoni mwa watazamaji waliokuwa wakiwashuhudia washiriki wa mbio hizo wakichuana.

Pamoja na kukumbwa na mkasa huo, Rotich alifanikiwa kumaliza mbio hizo akiwa wa kwanza na kushangiliwa na umati mkubwa wa mashabiki.

Hii ni mara ya pili kwa Rotich kushinda mashindano ya riadha nchini Brazil. Wiki iliyopita, mwanariadha huyo wa kimataifa wa Kenya aliibuka mshindi katika mbio za kimataifa za Sao Silvestre Race zilizofanyika mjini Sao Paulo.

Katika mbio za juzi, Mark Korir wa Kenya alishika nafasi ya pili, akifuatiwa na Daniel da Silva wa Brazil. Polisi wamesema Wallace na historia ya matatizo ya akili na kwamba hiyo haikuwa mara ya kwanza kujihusisha na matukio ya aina hiyo.

No comments:

Post a Comment