Maisha magumu yalichangia niwe 'teja'
Na Peter MwendaBAADA ya Msanii Ray C kujitokeza na kumshukuru Rais Jakaya Kikwete kwa kuchangia matibabu yake baada ya kuathirika na dawa za kulevya, msanii mwingine Abubakar Katwila a.k.a Q-Chilla au Chichi amejitokeza na kusema ugumu wa maisha na kukosa soko la kazi zake kulimfanya avute dawa za kulevya.
Akizungumza katika kipindi cha Makutano alisema pia kuna baadhi ya watu wa karibu walichangia hapo alipofikia baada ya kumwacha peke yake na kukabiliana na ugumu wa kazi hiyo.
Alisema watu hao walihakikisha kila anachofanya hakifanikiwi, mwisho alijikuta katika wakati magumu na kushindwa kujielewa amemkosea nani na nani amuombe msamaha.
Alisema anawashukuru watu wote wa karibu walihudhunishwa na hali yake na kumshauri vizuri "....wale ambao wameingia katika wimbi hilikwanza kabisa wajikubali kuwa wana tatizo na cha pili ni kumrudia muumba wetu, Mungu Mwenyezi..." alisema Chichi.
"Nampongeza Rais wetu Kikwete kwa kumsaidia msanii Ray C ambaye pia alikuwa katika mtego huu na kutoa mfano kuwa hata Rais Obama alimsaidia marehemu Whitney Houston , Rais wa Afrika Kusini Nelson Mandela alimsadia Brenda Fassie...." alisema.
Pia waliwashauri wasanii wote walioathirika na dawa za kulevya wajitokeze ili wasadiwe na jamii kwani bado inawahitaji.
"Sasa hivi nafanya muziki lakini nipo kimataifa zaidi kwani wanamuziki wengi nchini huishia kusikika nchini,"alisema
Alisema kwa sasa hana mpango wa kutoa albamu na kusema ataendelea kutoa nyimbo zitakazogusa jamii na kali.
Msanii huyo Desemba mwezi DFesemba mwaka jana alitangaza kuvuta dawa za kulevya kwa muda miaka miwili lakini akahuzunika na hali hiyo.
No comments:
Post a Comment