TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION

TANGAZO SHIWATA

Monday, 19 November 2012

SERIKALI WENYE MIGODI KUSAIDIA WACHIMBAJI WADOGO

 Na Peter Mwenda

WIZARA ya Nishati na Madini kushirikiana na Wachimbaji wakubwa wa madini wameazimia kusaidia wachimbaji wadogo kuwapatia vifaa vya kisasa vya uchimbaji na mafunzo.

Naibu Waziri wa Wizara ya Nishati na Madini, Stephen Masele akifungua mkutano wa wachimbaji wadogo na wakubwa wa madini nchini Dar es Salaam jana alisema Serikali imejipanga kuwainua wachimbaji wadogo wajiendeleze.

"Serikali inakutana na wadau wa sekta ya madini, wachimbaji wadogo, wachimbaji wakubwa na Benki ya Dunia kuangalia namna watakavyoshirikiana kuwanufaisha kwa kutoka mafunzo na wajue mchango wao kwa taifa" alisema Waziri Masele.

Alisema wachimbaji wadogo ni lazima watoke hapo walipo na kuwatoa hofu ya kukombea maeneo ya uchimbaji madini na kuwapatia leseni za kuwaruhusu kuchimba kihalali.

Waziri Masele alisema Wachimbaji wadogo pia wanatakiwa kuchangia pato la taifa kwa kulipa kodi,kushirikiana na wachimbaji wakubwa na kusaidia jamii.


"Imefika wakati kwa Serikali kuwaeleza wananchi mapato yanayotokana na madini na ijulikane kwa jamii inayozunguka machimbo ya madini wananufaikaje na madini hayo ikiwepo kujengewa shule, zahanati na huduma nyingine" alisema Waziri Masele.

Alisema Tanzania kuna wachimbaji wadogo zaidi ya milioni moja ambao kutumia mpango wa Ushirikiano kati ya Serikali na Sekta Binafsi (PPP)watanufaika kwa mikopo na kupata vifaa vya kisasa na uchimbaji.

Bw. Masele alisema machimbo mengine kama ya Geita wanatumia zebaki kuosha dhahabu yao ambayo ni hatari kwa afya yao na hiyo imekuwa ikifanyika katika mikutano hiyo na kidogo kidogo imeanza kueleweka.

Kamishna wa madini wa Wizara ya Nishati na Madini, Ali Samaje alisema migogoro kati ya wachimbaji wadogo na wakubwa na migogoro kati ya jamii na wachimbaji wakubwa vitakwisha.

Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa wachimbaji wadogo, Mwanne Ambari alisema Serikali inajitahidi kuleta karibu wachimbaji wadogo na wakubwa  kukaa pamoja na kushirikiana kusaidia jamii.
 

mwisho





No comments:

Post a Comment