TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION

TANGAZO SHIWATA

Tuesday, 20 November 2012

Rais apunguziwe madaraka

 Na waandishi Wetu
BAADHI ya wananchi wa wa Mkoa wa Dar es Salaam wametaka Katiba mpya isitoe nafasi ya wabunge kuteuliwa kuwa mawaziri na rais aondolewe madaraka ya kuteua viongozi,pia kusiwepo nafasi za wabunge wa Viti maalum.

Wakitoa maoni yao katika mkutano wa Kata ya Kurasini, Temeke jana Bw.Thomas Mayagilo alisema kuwepo kwa madaraka makubwa ya Rais yanamfanya ashindwe kupata nafasi ya kuwajibika ipasavyo na kushauri kuwa nafasi ya uteuzi ifanywe na Waziri Mkuu.

"Katiba Mpya ijayo itoe nafasi kwa waziri Mkuu kufanya uteuzi wa nafasi mbalimbali za viongozi ikiwa ni moja ya kumpunguzia majukumu Rais ambaye anatakiwa kutatua mbalimbali za wananchi zikiwemo kuonanan nao moja kwa moja" alisema Bw. Mayagilo.

Mwananchi mwingine Bw.Uliza Mohamed alisema katiba mpya iwajali wananchi hasa wanapopatwa na majanga ya kuunguliwa nyumba au kubomolewa nyumba zao kwa ajili ya upanuzi wa  barabara walipwe katika muda muafaka badala ya kupigwa danadana.

Naye Bw.Gidion Kaduma alisema kutokana na mgongano wa Wazinzar na watanmganyika kutokana na muungano alishauri kusiwepo na serikali mbili badala yake Serikali iwe moja itakayobeba jina la Tanzania tu.


Mwananchi huyo katika maoni yake menginea alisema Mahakama itoke kuwa katika mamlaka ya Rais katika kuteua majaji na kuwa yeye ndiyo msemaji wa mwisho badala yake kiwe chombo huru kinachojitegemea chenyewe.

 Pia wananchi hao wametaka kuwepo Tume Huru ya Uchaguzi ambayo itashirikisha wawakilishi kutoka vyama vyote vya siasa nchini ili kuondoa malalamiko ya kuonekana matokeo mbalimbali yamechakachuliwa.

Katika mkutano huo ulioongozwa na Mjumbe wa Kamati hiyo,ambaye aliwahi kuwa Waziri Mkuu wa Awamu ya Pili, Dkt.Salim Ahmed Salim wananchi hao pia walitaka wawekezaji wapewe miezi sita ya kufanya utafiti wa madini baada ya hapo waanze kuilipa kodi.

Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Kuratibu maoni ya Katiba Mpya, Suleiman Omar Ali aliwataka wanachi hao kutoa maoni yao bila hofu na kile wanachotaka kiwekwe kwenye katiba mpya kwa njia ya mikutano, kuandika kwa maandishi, njia ya simu ya mkononi na barua pepe.

mwisho


No comments:

Post a Comment