Baadhi ya waisilamu wa kijiji cha Dogo Dawa wakikimbia baada ya kushambuliwa wakati wakitoka msikitini.
Wakuu wa Nigeria wanasema kuwa watu waliokuwa na
silaha wamewauwa watu kama 20 katika shambulio lilofanywa alfajiri kwenye
kijiji cha Dogo Dawa katika jimbo la Kaduna kaskazini mwa nchi.
Waliouwawa wengi walikuwa wakitoka msikitini. Washambuliaji
walifyatua risasi na kuwapiga visu waliokuwako na tena walimuuwa mzee wa jamii
nyumbani kwake.
Afisa wa habari wa jimbo hilo, Saidu Adamu, aliiambia
BBC kwamba gengi la majambazi wa jimbo hilo walifanya mauaji hayo.
Alisema shambulio hilo ni la kulipiza hatua
iliyochukuliwa na wanakijiji cha Dogo Dawa ya kuunda kikosi cha wanamgambo wao
wenyewe kuwatimua majambazi hao ambao wamekuwa tishio kijijini.
|
No comments:
Post a Comment