TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION

TANGAZO SHIWATA

Saturday, 6 October 2012

TANZANIA ITAENDELEA KUTATUA MGOGORO KATI YAKE NA MALAWI


NA MAGRETH KINABO – MAELEZO
WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe amesema kuwa Tanzania itaendelea kutafuta msuluhishi wa mgogoro wa mpaka kati ya Malawi na Tanzania  kuhusu ziwa Nyasa  iwapo nchi hiyo haitaweza kuja kwenye meza ya mazungumzo  juu ya suala hilo kwa kuchukua hatua mbalimbali.
Mazungumzo ya mgogoro huo ambayo yangetarajiwa kuanzia Oktoba 7 hadi 10, mwaka huu, kinachotarajiwa kufanyika jijini Dares Salaam.
Aidha  Waziri Membe alitoa pendekezo kwa serikali  ya Malawi kwa kuiomba kuwa ikubali timu mbili zilizokuwa katika mazungumzo hayo zikaendelea kukutana ili kuweza kupendekeza msuluhishi  wa tatizo hilo kwa pamoja.
 Kauli hiyo ilitolewa leo  na Waziri huyo katika mkutano wake na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mara baada ya ziara kurejea  nchini hapa kutoka Canada  alipokuwa akihudhuria mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa usiku wa kuamkia leo  kuhusu  hatua  ya serikali ya  Malawi kuandika barua  mbili kwa serikali ya Tanzania mwishoni mwa mwezi uliopita.
Ambapo alisema wamesitushwa na uamuzi huo ,kabla ya kujibu barua hizo.
“Ikiwa Malawi hawatakuja katika meza ya mazungumzo tutaendelea kutafuta msuluhishi juu ya tatizo hili. Tumeamua kulimaliza suala hili chini ya uongozi wa Rais wa Awamu ya Nne ya Rais Jakaya Kikwete kwa kutumia timu za wataalamu tatu, ambazo ni  wakumbukumbu ambao wataishia kuchukuia kumbukumbu za maisha ya ziwa hili kabla na baada ya mwaka 1890 nchini Uingereza, pia kukupitia nyaraka mbalimbali itakazozitumia ”alisema . Waziri Membe.

No comments:

Post a Comment