Na Elizabeth John
MKURUGENZI wa Misitu na
Nyuki, chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii, Dk Felician Kilahama
(Pichani kushoto), amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Shughuli za Misitu
Duniani ambapo ataiwakilisha Afrika kwa kutumia bendera ya Tanzania,
chini
ya mfuko wa chakula na kilimo.
Akizungumza na waandishi wa
habari jijini Dar es Salaam jana, Kilahama alisema katika kikao cha 21 kilichohudhuriwa
na Kamati ya Shirika la Chakula na Kilimo Duniani (FAO), kilichofanyika nchini
Italia wiki iliyopita, kulingana na kanuni za utaratibu wa kamati, ikaamua kumchagua
Mwenyekiti kutoka miongoni mwa wanachama wake.
Kilahama alisema anajisikia
furaha sana kuchaguliwa katika idara hiyo na
kwamba Watanzania wanapaswa kutambua kuwa, hawakufanya makosa kumchagua yeye,
kwani ana uhakika bendera ya Tanzania
itapepea vema.
“Watanzania inatakiwa
mniombee kazi hii sio ndogo, kikubwa ambacho tutakuwa tukikifanya ni kuleta
maendeleo ya misitu, pamoja na kujua tutapunguzaje gharama za matumizi ya
nishati, kama kuni na mkaa bila kukata miti na
kupunguza misitu kitu ambacho kina athiri mazingira,” alisema Kilahama.
Alisema, kwa kawaida
anayetaka uongozi katika shirika hilo huwa anatuma barua ya maombi kwa uongozi
husika kwa kushirikiana na uongozi wa nchi yake, jina lake likipitishwa ndio
atachaguliwa na wanakamati wa shirika hilo.
“Kiukweli ilikuwa kama miujiza, aliyekuwa amechaguliwa alikuwa ni Mnigeria
alishindwa kutokana na sababu ambazo zipo nje ya uwezo wake na Mnamibia alikosa
viza ya kuingilia nchini Italia, hapo ndio nikachaguliwa mimi kwa asilimia
zaidi ya 120,” alisema.
Aliongeza kuwa, kazi hiyo
ataifanya kwa muda wa miaka miwili na amewataka Watanzania wamuombee katika
shughuli hizo ambapo anaimani itakuwa ni faida ya nchi nzima kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment