TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION

TANGAZO SHIWATA

Tuesday 9 October 2012

MAADHIMISHO YA SIKU YA POSTA DUNIANI



 Meneja Mkuu wa Biashara wa Shirika la Posta Tanzania, Kilala Sendama akizungumza katika Maadhimisho ya siku ya Posta Duniani.
Meneja Mkuu wa Biashara wa Shirika la Posta Tanzania, Kilala Sendama akimkabidhi mmoja wa washindi wa shindano la Uandishi wa Barua, Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Kifungilo, Alvinar Alexander Mgoye wakati wa maadhimisho ya siku ya Posta Duniani iliyofanyika jijini Dar es Salaam. (Picha na Francis Dande)
Washindi wa shindano la Uandishi wa Barua wakiwa katika picha ya pamoja
 

Na Mwandishi Wetu
SHIRIKA la Posta Tanzania limefanikiwa kupata tuzo maalumu ya kimataifa kutoka kwa Umoja wa Posta Duniani (UPU).

Mbali na hilo, shirika hilo limeanzisha vituo 36 vya kutoa huduma ya Internet katika maeneo mbalimbali nchini kwa lengo la kuboresha mfumo wa mawasiliano.
 
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam katika Maadhimisho ya siku ya Posta duniani, Meneja Mkuu wa Biashara Tanzania Kilala Sendama alifafanua kuwa, cheti hicho kimekuja baada ya shirika kupata alama ya 1,765 kati ya alama 2000 zilizokuwa zikishindaniwa.
 
“Cheti hicho kinadhibitisha ubora wa huduma zinazotolewa na kilikabidhiwa kwa Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi wa mashirika ya posta, Yamungu Kayandabila, vile vile tuzo hiyo itatumika kama kichocheo cha kuongeza ufanisi wa mafanikio zaidi” alisema Sendama.

 
Katika hilo alichanganua kuwa licha ya shirika kukabiliwa na changamoto lukuki katika utoaji huduma endelevu, lakini limekuwa miongozi mwa historia ya mabadiliko chanya hususani katika mtandao wa dunia kuanzia ngazi ya Kitaifa pamoja na Kimataifa.
 
Sendama alitabanaisha kwamba mbali na tuzo hiyo, shirika limetoa tuzo kwa Wanafunzi 10 katika shule za Sekondari nchini walioshinda vizuri katika shindano la Uandishi wa Barua kwa ngazi ya kitaifa kwa mwaka 2012.
 
Aidha, aliwataja washindi hao ni Alvinar Mgoye kutoka shule ya sekondari Kifungilo, Mary Kilapilo sekondari ya Usambara,Sonia Chiliko Kifungilo, wote wa Mkoani Tanga, Nyinga Jackson kutoka sekondari ya Ilboru Mkoani Arusha, pamoja na Anway Omary kutoka shule ya Azania Dar es Salaam.

 
Aliwataja wengine ni Violet Richard kutoka shule ya sekondari St Joseph Mkoani Mwanza, Edith Mkwawa, Sylcheria Kaole, wote kutoka Usambara Korogwe, Raya Mwamwetta kutoka Kifungilo Mkoani Tanga, pamoja na Faraj Azizi kutoka shule ya sekondari Ummu Salama Mkoani Iringa.

 
Akizungumza kwa niaba ya wanafunzi wenzake waliopewa tuzo hizo, Mary Kilapilo alitumia fursa hiyo kuwataka wanafunzi wengine kuipenda huduma hiyo kwa sababu inawapunguzia matatizo mbalimbali likiwemo la kutojiingiza katika vishawishi vya mapenzi.

No comments:

Post a Comment