KATIBU Mkuu wa Shirikisho la ngumi za Ridhaa
(BFT), Makore Mashaga amemtaka Promota wa ngumi za kulipwa nchini, Kaike Siraju
kuwalipa mabondia fedha zao kama walivyokubaliana kwa lengo la kuendeleza
mchezo huo hapa nchini.
Kaike anadaiwa kuwafanyia kitendo ambacho si cha
kiungwana mabondia chipukizi Issa Omar na Mwaite Juma kwa kuwapambanisha Julai 15 mwaka huu kwa
makubaliano ya kuwalipa na baadae kutowalipa.
Juni 25 mwaka huu Kaike aliwasainisha mkataba
mbele ya Katibu Mkuu wa Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBC), Ibrahim Kamwe kuwa
Omar kucheza na Ramadhan Kumbele kwa malipo ya sh. 80,000.
Pia Kaike alifanya hivyo kwa bondia, Juma aliyecheza na Anthony Mathias, ambapo vijana hao walicheza na hawakulipwa na promota huyo.
Akizungumza jijini Dar es
Salaam, Mashaga amesema kuwa kwa kufanya hivyo atawakatisha tamaa mabondia
wakiwa bado hawajawa na uzoefu katika mchezo huo, hivyo anamshauri awalipe
mapema.
Alisema kuwa mambo yaliyofanywa na promota huyo
si ya kiungwana ni kuwavunja moyo mabondia chipukizi, kudumaza ngumi na kufanya
mchezo wa ngumi uonekane ni mchezo wa wahuni kwa vitendo vya kihuni kama hivi.
No comments:
Post a Comment