Mwananafunzi wa shule ya Sinza Maalum akiimba wimbo
wa mwanamuzi Ambwene Yesaya (AY) walipotembelewa na mwanamuzi huyo
mwishoni mwa wiki hii wakiongozana na wafanyakazi wa Airtel, kushoto ni
meneja mahusiano wa jamii wa Airtel Hawa Bayumi, watatu kutoka kulia
Ambwene Yessaya (AY) akifwatiwa na Afisa uhusiano na matukio wa Airtel
Dangio Kaniki.
Student of Sinza Maalum performing a song of
R&B artist Ambwene Yessaya known as AY, when he visited the school
accompanied by Airtel staffs end of this week, left is Corporate Social
Responsibility Manager of Airtel Hawa Bayumi,, third from right is
Airtel ambassador Ambwene Yessaya followed by Public Relations and
Events officer of Airtel Dangio Kaniki.
Wafanyakazi wa Airtel wakiwa na balozi wao Ambwene
Yesaya katika picha ya pamoja na wanafunzi wa shule ya sinza Maalum
iliyopo jijini Dar Es Salaam walipotembelea shule hiyo mwishoni mwa wiki
hii kama mwendelezo wao wa kusaidia jamii kwa watoto wenye mahitaji
maalum kupitia mradi wao wa kuchangia Elimu kwa kushirikiana na
BAMVITA.
Staff s from Airtel with their ambassador Ambwene
Yessaya (AY) on a group picture with students from Sinza Maalum in Dar
Es Salaam when visited the school at the end of this week as part of
supporting schools with special needs in education through their
project who are working together with Bamvita
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kupitia
kitengo chake cha huduma kwa jamii imeanza mchakato wa kutembelea baadhi
ya shule zitakazonufaika na mradi maalum wa kuwasaidia watoto wenye
mahitaji maalum ili kujionea changamoto zinazowakabili pamoja na
kuwahimiza watanzania kuweza kuchangia mradi huo unaoendeshwa kwa
ushirikiano na Baraza la maendeleo ya vitabu Tanzania (BAMVITA).
Afisa mawasiliano na matukio wa Airtel Bi Dangio
Kaniki amesema kampuni hiyo ikiwa na Balozi wake msanii Maarufu AY
itatembelea shule zote zilizopo Dar es Salaam pamoja na mikoani na
kubaiunisha matatizo wanaoyokumbana nayo ili kuona namna ya kuwasaidia.
Amesema shule za wanafunzi wenye mahitaji maalum
zinahitaji vitendea kazi vingi ili kuwafanya wanafunzi hao kuweza
kupatiwa elimu inayostahili.
“Shule hizi zinamahitaji mengi sana, Airtel tumeona
ni vyema kumtumia pia Balozi wetu huyu msanii maarufu nchini A Y
kuendea kuwafikishia jamiii ujumbe waendelee kuchangia katika mradi huu
wenye lengo la kuendeleza jamii” alisema Bi DANGIO KANIKI Afisa
mawasiliano na matukio wa Airtel
Akizungumza mara baada ya kutembelea shule ya
msingi Sinza Maalum Balozi wa Airtel AMBWENE YESAYA (A.Y) amesema
kukamilika kwa mradi huo kutasaidia kuongeza kiwango cha elimu kwa
watoto wenye mahitaji maalum.
“Watoto hawa wenye uhitaji maalum nimejionea
mwenyewe kuwa wakiwezeshwa wanaweza, ndio maana naona ni vyema zaidi
kushirikiana na Airtel pamoja na jamii kwa ujumla kuhakikisha
tunawachangia vijana wetu hawa nao waweze kuendeleza hata vipaji vyao
pamoja na elimu yao.
Ninaomba kuwakubusha watanzania kuchangia katika
kuwapatia vijana hawa vifaa mbalimbali ambavyo ni changamoto kwao,
unaweza kuchangia kwa kupitia Airtel Money ambapo unaandika jina la
fumbo VITABU na utatuma kiasi chochote au kwa kutuma SMS yenye neno VITABU kwenda namba 15626 na atakuwa amechangia shilingi 200 tu.
Watanzania naomba tusaidiane katika elimu kwa kuwa
tuanaamini Tanzania itajengwa na sisi wenyewe. Alimalizia kusema
AMBWENE YESAYA ---Balozi wa Airtel.
Wakati wa ziara hio mwuishoni mwa wiki hii Mwalimu
Mkuu wa shule ya Sinza Maalum, SIMON Milobo alibainisha kuwa shule hiyo
inakabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwemo uhaba wa vifaa vya
kufundishia pamoja na mafuta ya kuendeshea gari la wanafunzi.
Kampeni ya Airtel kwa
kushirikiana na Bamvita itaendeshwa kwa muda wa miezi mitatu , na
Watanzania wataweza kuchangia kwa kutuma neno “Vitabu” kwenda namba 15626 na kwakufanya hivyo kila SMS utakayotuma utakuwa umechangia shilingi 200 itakayoingizwa katika mradi huu”
No comments:
Post a Comment