TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION

TANGAZO SHIWATA

Friday, 28 September 2012

UJIO WA MAOJA WASHTUA JIJI LA WINDHOEK NCHINI NAMIBIA




AINGIA KWA MBEMBWE ZA AINA YAKE
AKATAA KUKUMBATIANA NA WAGENI WAKE UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA HOSEA KUTAKO, WINDHOEK, NAMIBIA
 
BONDIA Mtanzania, Rajabu Maoja, amelitingisha jiji la Windhoek, nchini Namibia, alipowasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Hosea Kutako. 

Maoja aliingia kwa mbemwe za aina yake na kugoma kukumbatiana na wenyeji wake ambao walikuwa na shahuku kubwa ya kumlaki wakati wa mapokezi yake kwa kumkumbatia.
 
Akiwa na sura ya kujiamini huku akitembea kibabe Mtanzania Maoja, alionyesha nia ya kuuchukua mkanda wa ubingwa wa IBF katika bara la Afrika wakati atakapoumana na bingwa wa Namibia Gottlieb Ndokosho kesho siku ya Jumamosi.
 
Mpambano huo ulipewa jina la Vita Vya Jangwa wa Kalahari (The Battle for the Kalahari Desert) na waandaaji wake ambao ni kampuni ya Kinda Boxing Promotions inayoongozwa na Simon Nangolo limeleta shamrashamra za aina ya pekee katika ukanda huu wa Kusini mwa jangwa la Sahara.
 
Mpambano huo ni moja ya mapambano ambayo yapo kwenye programu ya Utalii wa Michezo ya IBF (IBF Sports Tourism) ambayo inasimamiwa na Shirikisho la Ngumi la Kimataifa (IBF) na kuratibiwa na Rais wa IBF katika bara la Afrika, Mashariki ya Kati na Ghuba ya Uajemi, Mtanzania Onesmo Alfred McBride Ngowi.
 
Nao mabondia kutoka Zimbabwe na Afrika ya Kusini ambao watacheza mapambano ya awali wameshafika na tayari shamrashamra za mpambano huo zimeshika kasi kwa wadau na wapenzi wa ngumi wa nchi ya Namibia na nchi jirani kama Botswana, Afrika ya Kusini, Lesotho na Swaziland.
 
Hii ni mara ya kwanza kwa ushandani mkubwa namna hiyo kuwahi kutokea katika jiji la Windhoek hapa Namibia.
 
Mpizania wa Maoja Gottlieb Ndokosho ameingai mitini na hajaonekana tangu tuingie katika jiji hili la maraha!
 
Kesho  ni kesho na Watanzania wamuombee mwakilishi wao ili aweze kuipeperusha vizuri bendera ya Tanzania!
 
Mungu mbariki Rajabu Jumanne Maoja, Mungu ibariki nchi nzuri ya Tanzania.
 
Imetolewa na: Uongozi
Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBC) 

No comments:

Post a Comment