BAADA
ya kutamba na ngoma yake inayokwenda kwa jina la ‘Utanikumbuka’, Mkali
wa muziki wa kizazi kipya nchini, Ismail Seif ‘Suma Lee’ anajipanga
kuachia kibao chake kipya kinachokwenda kwa jina la ‘Skendo’.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam jana, Suma Lee alisema yupo katika hatua za mwisho
za uandaaji wa kazi hiyo ambayo anaamini itakua gumzo mtaani kutokana
na ujumbe ambao wimbo huo umebeba.
“Wimbo
huu unaujumbe mzito kwa jamii hasa kwa dada zetu wa kisasa ambao
wanapenda kuvaa nguo ambazo sio maadili ya watanzania kwa kisingizio
kwamba ni utandawazi,” alisema Suma Lee.
Suma
Lee alisema anawashukuru mashabiki wake kwa kumpokea vizuri katika
tasnia ya muziki wa kizazi kipya kitu ambacho kinampa nguvu ya kuendelea
kufanya kazi na kutoa nyimbo ambazo zinakua na ujumbe kwa jamii.
Mbali
na nyimbo hizo Suma Lee alishawahi tamba na vibao vyake kama, Chungwa,
Hakunaga na nyinginezo ambazo zilimtambulisha na kufanya vizuri katika
tasnia ya muziki wa kizazi kipya nchini.
No comments:
Post a Comment