TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION

TANGAZO SHIWATA

Sunday, 30 September 2012

Jumba la EBSS-2012 linatisha kwa uzuri




huu ndio mlango wa kuingia ndani ya mjengo wenyewe, Madam Ritta anaingia hapa....


 
SHINDANO la kusaka vipaji vya uimbaji la Bongo Star Search limeanza tena, ambapo mwaka huu itakuwa na washiriki 12 na mmoja wao atakayeshinda ataibuka na kitita cha Shilingi MIlioni 50.
Kila mwaka shindano hili ninazidi kuboreshwa na kuwa na muonekano bora, safari hii shindano hilo linafahamika kama Epiq Bongo Star Search (EBSS) kutokana na kampuni ya Simu ya Zantel kuamua kuunga mkono kwa kutoa ufadhili.
Kwenye maboresho ya EBSS washiriki wote 12 watakuwa wakiishi katika nyumba moja, wakiwa ndani watafanya kazi mbalimbali pamoja na kupata mafunzo ya muziki kutoka kwa wakufunzi wenye utaalamu wa masuala ya muziki.
Jaji Mkuu wa EBSS Ritta Paulsen maarufu kama `Madame Ritta'alisema jumba hilo lenye kila kitu ndani ni moja ya alama kuu ya maboresho ya shindano hilo na kuwa la Kimataifa zaidi.
"Jumba la EBSS ni moja ya nyumba yenye ubora nchini, washiriki wataishi humo kwa muda wa wiki nane wakati kusaka msindi wetu, wakiwa ndani watafurahi, watajifunza mambo mbalimbali pamoja na kuongeza uzoefu wa kuishi kwa kujituma," alisema Ritta.
Ufunguzi wa jumba hilo ulifanyika mapema wiki hii, ambapo watu mbalimbali wakio\wemo viongozi wa Zantel walishuhudia sherehe ya uzinduzi.
ENEO ILIPO EBSS HOUSE
Jumba hilo la kifahari  lipo katika eneo la Kawe Mzimuni, imezungukwa na majumba ya kifahari pamoja na kambi ya Jeshi ya Lugalo.
Sehemu hiyo ni tulivu, kitu ambacho kinasababisha washiriki kujifunza vizuri wakiwemo ndani ya nyumba pamoja na kufanya shughuli zao kwa utulivu mkubwa.
NDANI YA NYUMBA.
Ukumbi wa mazoezi: Mara unapoingia ndani kupitia lango kuu wenye kunakshiwa na marembo ya Kizanzibar, utakumbana na chumba kikubwa, ambapo hapo ndipo sehemu maalum ya kufanyia mazoezi ya uimbaji.
Kwenye chumba hicho kuna vyombo mbalimbali vya muziki vitakavyotumiwa na washiriki wakati mazoezi yao ya vitendo.
Dadasa: Kwa upande wa kushoto ndani ya jumba hilo kuna chumba kidogo chenye viti pamoja na ubao. Kwa mujibu wa Muandaaji wa Shindano hilo Ritta paulsen chumba hicho kitatumika kama darasa, washiriki watapewa mafunzo mbalimbali ya jinsi ya kutumia toni za muziki kwa nadharia.
Jiko: Upande wa mbele kabisa kuna chumba maalum kwa ajili ya kupikia, humo kuna vifaa vyote vya mazuala ya upishi, hivyo itakuwa rahisi kwa washiriki wenyewe kupika chakula wanachotaka endapo hawatapenda kula vile wanavyopikiwa na wapishi maalum waliokuwemo ndani ya nyumba.
Vyumba vya kulala washiriki: Katika shindano hilo kunakuwa na mtu ambaye anaitwa Mkuu wa nyumba, huyu ni mshiriki ambaye ameshinda kutokana na kufanya jitiahada kubwa katika kazi zake na hukabidhiwa kazi ya kuwaongoza wenzake. Safari hii Mkuu wa nyumba atakuwa na chumba chake cha kulala chenye kila kitu ndani yake, hivyo anaweza kujifanyia shughuli zake hata akiwa ndani ya chumba chake. Kwa upande wa washiriki kuna chumba kikubwa chenye vitanda vitakavyowatosheleza kulala washiriki wote.
Vitu Vingine: Baadhi ya vitu vingine vilivyokuwemo kwenye nyumba hiyo ni pamoja na bwawa la kuogelea, chumba cha kulia chakula, sehemu ya kupumzikia pamoja na bustani nzuri ya kufanyia mazongezi.
Washiriki waliofanikiwa kuingia ndani ya nyumba hiyo ni Godfrey Kato, Husna Nassoro, Linias Mhaya, Menynah Atiki, Norman Severina, Nsami Nkwabi, Nshoma Ng'hangasamala, Salma Mahin, Vicent Mushi, Wababa Mtuka na walter Chilambo.

No comments:

Post a Comment