TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION

TANGAZO SHIWATA

Monday, 24 September 2012

BAO WAOMBA UDHAMINI MASHINDANO YA MWL JK NYERERE



Na Elizabeth John
SHIRIKISHO la Mchezo wa Bao Tanzania (SHIMBATA), limewaomba wadau kujitokeza kudhamini mchezo huo ili kufanikisha kuendesha shindano la kumuenzi Baba wa Taifa Mwl. JK Nyerere, ambalo limepangwa kuanza Octoba 10 hadi 13 Mkoani Shinyanga.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Rais wa SHIMBATA, Monday Likwepa alisema hadi sasa hawana ufadhili wowote ambao umejitokeza kudhamini ili kufanikisha mashindano hayo, ambayo yatashirikisha mikoa 11 ya Tanzania bara na mmoja kutoka visiwani Zanzibar.
“Gharama ambazo zitatuweza kufanikisha mashindano hayo ni milioni 59, ambapo zitakuwa ni gharama za wachezaji wa mikoa yote kwa huduma za maradhi na chakula ambapo kila Mkoa utaleta wachezaji sita,” alisema Likwepa.
Mbali na mashindano hayo, SHIMBATA wameandaa mikakati endelevu ikiwemo uundwaji wa vyama vya mikoa, uendeshaji wa mashindano mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kushiriki mashindano ya kimataifa.
“Mchezo wa Bao ni Mchezo wa Kitanzania tena wa Kizalendo na ndio mchezo pekee uliosaidia harakati za kudai Uhuru wa Tanganyika kwa upande wa Bara na Visiwa vya Zanzibar kama eneo muhimu la kukutania kupanga mikakati ya kuung’oa ukoloni. Hivyo unatakiwa upewe heshima ya kutosha,” alisema Likwepa.
Aliongeza kuwa SHIMBATA wameanza majadiliano ya kuuingiza katika orodha ya michezo inayotumia akili zaidi Duniani kutoka Chama cha Kimataifa (IMGA) na kwamba wana uhakika wa kuchukua medali za mchezo huo ikiwa mwaka 2016 utafanikiwa kuingizwa katika mashindano ya Olimpiki.

No comments:

Post a Comment