TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION

TANGAZO SHIWATA

Monday, 6 August 2012

TANZANIA YAPATA NAFASI YA KUKAGUA HESABU ZA UN



Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali (CAG) ambaye pia ni Mkaguzi wa hesabu za Umoja wa Mataifa  (UN) Ludovick Utouh akiongea na waandishi wa habari kuhusu  Taasisi 10 za UN ambazo zitafanyiwa ukaguzi chini ya usimamizi wake ambapo watumishi 60 kutoka ofisini yake watafanya kazi hiyo. Kwa kipindi cha miaka sita nchi za Tanzania, China na Uingereza zimepewa jukumu la ukaguzi  wa hesabu za UN.
Picha na Anna Nkinda – Maelezo
Edwin Rweyumamu kutoka ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali (CAG)  akimkaribisha CAG ambaye pia ni Mkaguzi wa Hesabu za Umoja wa Mataifa (UN) Ludovick Utouh ili aweze kuongea na waandishi wa habari kuhusu  Tanzania kupata nafasi ya kukagua hesabu za UN kwa kipindi cha miaka sita. Watumishi 60 kutoka ofisi ya CAG  watafanya kazi ya kuzikagua taasisi 10 za UN.

No comments:

Post a Comment