Na Mwandishi Wetu
TAMASHA la watani wa Jadi Simba na Yanga Veteran litakalofanyika uwanja wa Bandari temeke maandalizi ya mchezo huo na mingine itakayopamba burudani hizo yamekamilika.
Mwenyekiti wa Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA), Cassim Taalib alisema kutakuwa na pambano la ngumi la uzani wa juu (Heavy Weight) kati ya Alfonce Mchuatumbo ns David Mlope (Zola D King) la raundi nane ambalo litatanguliwa na mengine kati ya Selemani Galile na Zumba Nkukwe la raundi nane na Nussa Sunga atacheza na Mussa Seif (Bodaboda).
Pia kutakuwa na michezo ya farasi na mbwa wa Jeshi la Polisi Tanzania ambao wataonesha kuruka vihunzi, kukamata wahalifu,kupiga saluti, kutambaa(Crow) na michezo mingine ya kujihami.
Ofisa Mnadhimu wa Kikosi cha Farasi na Mbwa, Bakari Ng'ulungo alisema jana kuwa maonesho hayo yatavutia watu wengi ambao hawajawahi kuona vitimbwi vinavyoneshwa na wanyama hao.
Tamasha hilo ambalo ni maalum kwa ajili ya kutafuta fedha za kujenga nyumba za wasanii katika kijiji cha Mwanzega, Mkuranga litaanza saa nne asubuhi na kuendelea mpaka saa 2 usiku.
Kiingilio kitakuwa sh. 1,000 kwa watoto,sh. 2,000 kwa watu wazima na sh. 5,000 kwa VIP..
No comments:
Post a Comment