
Vifaa
hivyo ambavyo ni jezi, bukta na soksi 20, vizibao (bibs) 20 na mipira
miwili vimekabidhiwa leo (Julai 12 mwaka huu) kwa Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF) na Ofisa Uhusiano wa kampuni hiyo, Amisa Juma.
Akikabidhi
vifaa hivyo, Amisa amesema wamefanya hivyo ikiwa ni sehemu ya mchango
wao kwa jamii lakini vilevile wameamua kuiunga mkono timu hiyo ambayo
wanajua haina mdhamini kutokana na vipaji na uwezo ambao umekuwa
ukioneshwa na wachezaji wake.
Pia
amezitaka kampuni, taasisi, watu binafsi na Serikali kuiunga mkono timu
hiyo ili iweze kufanya vizuri kwenye mashindano mbalimbali inayotarajia
kushiriki.
No comments:
Post a Comment