MUIGIZAJI
nyota wa filamu nchini Jacqueline Massawe ambaye ni maarufu kwa jina la
WOLPER amesisitiza kwamba amebadili dini na kwa sasa anajiandaa kwa
kuupokea na kufunga mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Akizungumza
katika chombo kimoja cha habari Luninga WOLPER amesisitiza kwamba yeye
hivi sasa ni muislamu na amejitayarisha kufunga na kujizuia kufanya
shughuli za kisanii ambazo zitamsababishia kutengua saum yake hivyo kwa
kipindi hicho cha muda wa mwezi mmoja atakuwa akijishughulisha na kazi
zake zingine.
"Unajua
dini ni imani na hii iko ndani ya moyo wangu hivyo nachukizwa kwa
kitendo cha baadhi ya ndugu zangu wa karibu kuniita MALAYA na hukumu kwa
mambo mbalimbali mimi ndiyo najua na fanya nini katika maisha
yangu"alisema.
Aidha
amewatupia dongo wale wote wanao mmtupia maneno ya kumdhihaki kwamba
hatoweza kufunga na kuswali , "Unajua tumepewa miezi 11 ambayo tuko huru
kufanya mambo mbalimbali ya starehe za kidunia kwanini nishindwe
kujizuia ndani ya mwezi mmoja tu, mimi nasema hivi nitasali sitakuwa na
makucha , manywele na mambo mbalimbali ambayo hayapendezi katika ibada
"

No comments:
Post a Comment